Mikhail Kalashnikov: Mbunifu wa kifo au shujaa wa Urusi?

Mikhail Kalashnikov: Mbunifu wa kifo au shujaa wa Urusi?

Ak 47 Chuma kinachokohoa kirusi ,moja kati ya kazi Urusi itajivunia.
Acha Raia wachache wapinge lakini mioyoni mwao wanaOna ushujaa wa Mikhail Kalashnikov Na ndio maana serikali ya urusi imeamua kukaa mbali na unafiki.
 
Ni kweli usemavyo ila inasikitisha sana unapowaona IS wakiitumia hiyo silaha kuua watu wasio na hatia
Hata zilivyoletwa kwa makundi ya waasi Kama D.R Conco, Rwanda, Burundi, C.A.R, na kwa wavuta bangi wa Sierra Leone waliowaua watu wasio na hatia.
 
Yup ni hizohizo hawana silaha mpya kenge hawa toka tunazaliwa mpaka tunazeeka tuna ona wanabeba hizi AK 47
Hawa wetu wanatumia SMG mpaka vitako vilishapasuka.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyo ni shujaa wa russia. Kwa sababu zana za kivita na bunduki ziko aina nyingi hata kabla ya yeye kuvumbua zilikwepo. Kwahiyo yeye asingevumbua AK47 bado kusingeleta amani duniani au maangamizi yasingeepukika.

Wa kumlaumu ni aliyeweka nchi na mipaka duniani na aliyevumbua silaha ya kwanza kwasababu hao ndio walioleta migogoro duniani. Dunia ingekuwa nchi ya amani unatembea kila mahali na na kujikimu.
 
Huyu jamaa ,,urusi wanamuhesabu kama Baba wa Siraha ..

Karibu bunduki nyingi zilizopo Urus nikutokana na ugunduzi wake.

Bongo Bahati mbaya.

Inawezekana akawa ndugu yako maana hayo majina kama yamefanana
 
Ni swali linalofikirisha kidogo usipofikiri kwa kina linaweza kukushinda kulijibu, lakini ukweli unabaki palepale mbunifu wa kifo ni Mungu pekee. Ubunifu ni nini? Kwa tafsiri yangu ubunifu ni kufanya kitu tofauti ambacho wengine wameshindwa kufanya. Kabla ya 1947; watu walikuwa wanatumia silaha, lakini AK 47 ikaja kuleta mapinduzi ya silaha. AK 47 hii ni silaha hatari sana, kwa hiyo jamaa ni mbunifu kwa sababu kwa wakati huo aliweza kufanya kitu tofauti ambacho wengine walishindwa kufanya. Lakini pia jamaa ni shujaa siyo kwa taifa lake tu bali hata kwa wale wote wanaoitumia silaha ya AK 47, Kalashnikov ndiyo shujaa wao.
 
Moja ya siraha hatari sana duniani na pia ni siraha iliyondoka na maisha ya watu wengi sana duniani.nchi karibu zote duniani zilitumia siraha hii.waasi na magaidi wote wametumia siraha hii.uyu jamaa naimani moto wake uko alipo sio moto wa kawaida
 
aliwahi kusema kuwa aligundua AK47 kwa ajili ya kulinda taifa lake dhidi ya uvamizi na ndio lengo lake la. msingi. sasa hayo matumizi mengine hasa wenye matukio ya kigaidi haikuwa dhamira yake
 
Back
Top Bottom