Ni swali linalofikirisha kidogo usipofikiri kwa kina linaweza kukushinda kulijibu, lakini ukweli unabaki palepale mbunifu wa kifo ni Mungu pekee. Ubunifu ni nini? Kwa tafsiri yangu ubunifu ni kufanya kitu tofauti ambacho wengine wameshindwa kufanya. Kabla ya 1947; watu walikuwa wanatumia silaha, lakini AK 47 ikaja kuleta mapinduzi ya silaha. AK 47 hii ni silaha hatari sana, kwa hiyo jamaa ni mbunifu kwa sababu kwa wakati huo aliweza kufanya kitu tofauti ambacho wengine walishindwa kufanya. Lakini pia jamaa ni shujaa siyo kwa taifa lake tu bali hata kwa wale wote wanaoitumia silaha ya AK 47, Kalashnikov ndiyo shujaa wao.