Mikoa 10 Inayoongoza kwa Uzalishaji wa Chakula Tanzania

Mikoa 10 Inayoongoza kwa Uzalishaji wa Chakula Tanzania

Tanga ,mahindi tunayo ya kutosha ,viazi ,machungwa ,,nyanya,Maharage halafu tupitwe na Dodoma 😀😀sio kweli bhana
😂Huko ni matunda mkuu mazao ya chakula huwezi kufaninisha na mikoa mingine
 
Hauifahamu dodoma, inatosha kusema hivyo

Ata huko kibaigwa hupafahamu, kondoa chemba huko hali yake ya hewa huijui, bahi ya mpunga kwako ni msamiati, chamwino ya uwele, mtama, mahindi, ufuta, karanga nk kwako ni tafsiri ya jangwa. Mpwapwa ya karanga, mahindi, albeit nk si kitu kwako
Wanaichukuliaga juu juu tu wanavyoinona wakiwa barabarani.
 
Hauifahamu dodoma, inatosha kusema hivyo

Ata huko kibaigwa hupafahamu, kondoa chemba huko hali yake ya hewa huijui, bahi ya mpunga kwako ni msamiati, chamwino ya uwele, mtama, mahindi, ufuta, karanga nk kwako ni tafsiri ya jangwa. Mpwapwa ya karanga, mahindi, albeit nk si kitu kwako
Umenena vyema. Wengi wetu tumekaririshwa kwamba Dodoma ni jangwa hakuna mvua. Kwa tafsiri hiyo basi tunafikiria hakuna kitu kinachoota Dodoma. Uhalisia si hivyo na watu waishio katika Mkoa huo wanalijua hilo. Karibu mjionee wenyewe kuhusu ukweli huu.
 
Dodoma aise Kuna mazao sana aise ukiingia huko chemba, kibaigwa utajionea Dodoma si jangwa ni bustani iliyobarikiwa
 
Habari za wakati huu wakuu,
Leo tunawaletea mada muhimu kuhusu "Mikoa 10 Inayoongoza kwa Uzalishaji wa Chakula Tanzania". Tanzania imebarikiwa na ardhi yenye rutuba na hali ya hewa inayofaa kwa kilimo, na mikoa mbalimbali imejipambanua katika uzalishaji wa mazao ya chakula.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Usalama wa Chakula Tanzania Bara ya mwaka 2024, mikoa ifuatayo imeonekana kuwa na uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula:

1. Ruvuma: Inajulikana kwa uzalishaji mkubwa wa mahindi, ikichangia kiasi kikubwa katika akiba ya chakula nchini.

2. Iringa: Pamoja na uzalishaji wa mazao ya chakula, mkoa huu una utoshelevu wa chakula kwa asilimia 139.

3. Njombe: Mkoa huu umeorodheshwa miongoni mwa mikoa yenye uzalishaji wa kutosheleza wa mazao ya chakula nchini.

4. Mbeya: Inajulikana kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula, ikiwa ni pamoja na mahindi na mboga mboga.

5. Morogoro: Mkoa huu ni maarufu kwa uzalishaji wa mpunga na mazao mengine ya chakula.

6. Kagera: Inajulikana kwa uzalishaji wa ndizi, kahawa na mazao mengine ya chakula.

7. Kigoma: Mkoa huu unazalisha mazao kama vile mihogo, mahindi na maharage.

8. Mara: Inajulikana kwa uzalishaji wa mahindi, mpunga na mazao mengine ya chakula.

9. Dodoma: Pamoja na kuwa makao makuu ya nchi, mkoa huu unazalisha mazao kama vile zabibu, mtama na mahindi.

10. Manyara: Mkoa huu umejipambanua katika uzalishaji wa mazao ya chakula, hasa mahindi na maharage.

Ni muhimu kutambua kuwa, licha ya uzalishaji huu mkubwa wa chakula, baadhi ya mikoa bado inakabiliwa changamoto za lishe duni, hususan udumavu kwa watoto. Hii inaonyesha umuhimu wa si tu kuzalisha chakula kwa wingi, bali pia kuhakikisha lishe bora na matumizi sahihi ya chakula hicho.

Vyanzo vya Taarifa Hii:

1. Bunge la Tanzania: parliament.go.tz

2. Nukta Habari: nukta.co.tz

3. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS): nbs.go.tz

Kwa yeyote anayetaka uchambuzi zaidi wa takwimu hizi, tafadhali tembelea tovuti hizo kwa taarifa kamili.

Wadau,Karibuni tujadili na kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuboresha zaidi sekta ya kilimo na kuhakikisha lishe bora kwa Watanzania wote.
Bila Shinyanga kuwemo hiyo orodha ni fake! Kila mwaka Shinyanga inaongoza kuzalisha mpunga!
 
Hii article iliibua zogo kubws kwenye matunda aina ya mananasi na maembe kwa sababu mazao hayo mkoa wa Dar es salaam uliongoza hii imekaaje mkuu. Kwenye haya mazao mawili
Kuna ukakasi sana hapo Dar.
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Hii ni uongo eti Dar inaongoza kwa kilimo cha Nanasi na Maembe hayo mashamba yako wapi? Hapo wamechukua ya kwenye masoko yaliyotoka mikoani huko. Dar hailimi zao lolote labda kidogo minazi
🤣🤣🤣 maembe na mananasi yanalimwa sana buguruni.
 
Dodoma kwenye Kilimo hapo ni uongo hata Hayo Mahindi unayaona hapo Kondoa mengi yanatoka Handeni Tanga labda karanga na Zabibu
Hilo ndio tatizo la kukariri kuwa eti Dodoma ni Jangwa😆😆..
-hivi unajua Dodoma ndio mkoa pekee wenye Soko la kimataifa la mahindi+nafaka Kibaigwa
-hivi unajua Dodoma ni mkoa unaoongoza Tanzania kwa kilimo cha Alizeti,Ufuta,Zabibu,Karanga,Uwele,Ulezi,Mbaazi,Tende,Rosella,Mtama
-hivi unajua mchele/mpunga unaozalishwa wilaya ya Bahi ni grade one /top class (ukienda soko lolote uliza mchele wa Bahi utajiwe bei yake)
-hivi unajua Dodoma ni mkoa wa pili baada ya Ruvuma kwa kujengwa maghala(vihenge) ya kuhifadhia mahindi yaliyo chini ya NFRA,WFP,FAO
-hivi unajua ranchi ya mifugo Kongwa ni ya pili kwa ukubwa katika Afrika
 
dodoma unaongoza kwa ufuta tanzania? mkuu hii takwimu ya wapi
 
Mangi unatudanganya mpaka Basi Dodoma kwa Kilimo ni uongo kabisa ila sababu kuna ghala la nafaka ndio wanadhani hivyo Alizeti inajulikana ni Singida halafu ulivyo muongo ina maana Mifugo iliyopo Dodoma inaweza kuzidi Mwanza,Geita au Manyara
 
Alizeti inajulikana ni Singida
Singida na Dodoma ni top producers wa Alizeti apa Tanzania na ndio mikoa yenye idadi kubwa ya viwanda vya kukamua mafuta ya Alizeti (Infact kiwanda kikubwa kuliko vyote kipo Veyula-Dodoma).
Naona unabisha ilimradi uonekane na wewe unabishana😆😆. Hoja yako ulisema Dodoma hakuna kilimo kutokana na ujangwa. Sasa nikuulize huko jangwani wanawezaje kuwa kwenye top list kwa kilimo cha Alizeti,Zabibu,Ufuta,Mtama,Ubuyu,Uwele,Castor Oil,Mbaazi,Ulezi,Tende,Rosella n.k
Mifugo iliyopo Dodoma inaweza kuzidi Mwanza,Geita au Manyara
-Dodoma wana ranchi kubwa ya mifugo ya pili kwa ukubwa katika Afrika inaitwa NARCO-KONGWA
-Dodoma ndio mkoa pekee wenye viwanda vya kusindika nyama (mpaka sasa vipo vitano)
-Dodoma ndio mkoa pekee wenye mnada wa kimataifa wa mifugo(Kigwe-Bahi) unaohudumia Afrika Mashariki na Kati
 
Back
Top Bottom