Yawezekana ikawa sio namba 1 lakini kwenye top 5 kati ya mikoa 31 ya Tanzania ipo.Nipe takwimu zako ambazo zinaitoa Dodoma kwenye top list ya uzalishaji wa Ufuta pamoja na mazao mengine niliyoyataja mfano Alizeti,Tende,Rosella,Zabibu,Ubuyu,Mbaazi,Ulezi,Uwele,Mtama,Karanga,Njugu n.k.dodoma unaongoza kwa ufuta tanzania? mkuu hii takwimu ya wapi
Hoja yangu ni kua dodoma sio mkoa unaoongoza kwa zao la ufuta, kama ulivosemaYawezekana ikawa sio namba 1 lakini kwenye top 5 kati ya mikoa 31 ya Tanzania ipo.Nipe takwimu zako ambazo zinaitoa Dodoma kwenye top list ya uzalishaji wa Ufuta pamoja na mazao mengine niliyoyataja mfano Alizeti,Tende,Rosella,Zabibu,Ubuyu,Mbaazi,Ulezi,Uwele,Mtama,Karanga,Njugu n.k.
Hoja ya mwenzako mwanzo ilikua Dodoma ni mkoa wenye ukame+jangwa na hakuna kilimo ...sasa amepata ukweli halisi kutoka "field"Hoja yangu ni kua dodoma sio mkoa unaoongoza kwa zao la ufuta, kama ulivosema
Kwanza huyu kama anongelea parachichi basi kaanza kuishi njombe juzi, hakuna sehemu inazalisha viazi kama njombe Tanzania nzima, Samaki ilikuwa iringa yote hiyo....😂Mkuu Njombe ni mzalishaji namba moja wa viazi Tanzania
NAtumai atakua amekuelewa mkuuHoja ya mwenzako mwanzo ilikua Dodoma ni mkoa wenye ukame+jangwa na hakuna kilimo ...sasa amepata ukweli halisi kutoka "field"
Ni kweli mkuu unakuta mtu hajatalii Njombe kabisa, ila Iringa pia ni mzalishaji wa Nyanya kwa wingi TanzaniaKwanza huyu kama anongelea parachichi basi kaanza kuishi njombe juzi, hakuna sehemu inazalisha viazi kama njombe Tanzania nzima, Samaki ilikuwa iringa yote hiyo....
Yaaah ilula nyanya ni nyingi sana, njombe miaka ya hivi karibuni ilibyogawiwa kutoka iringa ndio watu wanakata miti wanapanda parachichi....Ni kweli mkuu unakuta mtu hajatalii Njombe kabisa, ila Iringa pia ni mzalishaji wa Nyanya kwa wingi Tanzania
Ni kweli mkuu pia nadhani mazingira ya Njombe ndio yanasaidia upatikanaji wa hayo mazao kwa wingiYaaah ilula nyanya ni nyingi sana, njombe miaka ya hivi karibuni ilibyogawiwa kutoka iringa ndio watu wanakata miti wanapanda parachichi....
Pamoja na watu kupondea Dodoma ila ni Moja ya Mikoa muhimu Kwa uzalishaji hapa Tanzania na imeonesha wazi stori za watu waliokaririshwa ujinga wa vijiweni.Habari za wakati huu wakuu,
Leo tunawaletea mada muhimu kuhusu "Mikoa 10 Inayoongoza kwa Uzalishaji wa Chakula Tanzania". Tanzania imebarikiwa na ardhi yenye rutuba na hali ya hewa inayofaa kwa kilimo, na mikoa mbalimbali imejipambanua katika uzalishaji wa mazao ya chakula.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Usalama wa Chakula Tanzania Bara ya mwaka 2024, mikoa ifuatayo imeonekana kuwa na uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula:
1. Ruvuma: Inajulikana kwa uzalishaji mkubwa wa mahindi, ikichangia kiasi kikubwa katika akiba ya chakula nchini.
2. Iringa: Pamoja na uzalishaji wa mazao ya chakula, mkoa huu una utoshelevu wa chakula kwa asilimia 139.
3. Njombe: Mkoa huu umeorodheshwa miongoni mwa mikoa yenye uzalishaji wa kutosheleza wa mazao ya chakula nchini.
4. Mbeya: Inajulikana kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula, ikiwa ni pamoja na mahindi na mboga mboga.
5. Morogoro: Mkoa huu ni maarufu kwa uzalishaji wa mpunga na mazao mengine ya chakula.
6. Kagera: Inajulikana kwa uzalishaji wa ndizi, kahawa na mazao mengine ya chakula.
7. Kigoma: Mkoa huu unazalisha mazao kama vile mihogo, mahindi na maharage.
8. Mara: Inajulikana kwa uzalishaji wa mahindi, mpunga na mazao mengine ya chakula.
9. Dodoma: Pamoja na kuwa makao makuu ya nchi, mkoa huu unazalisha mazao kama vile zabibu, mtama na mahindi.
10. Manyara: Mkoa huu umejipambanua katika uzalishaji wa mazao ya chakula, hasa mahindi na maharage.
Ni muhimu kutambua kuwa, licha ya uzalishaji huu mkubwa wa chakula, baadhi ya mikoa bado inakabiliwa changamoto za lishe duni, hususan udumavu kwa watoto. Hii inaonyesha umuhimu wa si tu kuzalisha chakula kwa wingi, bali pia kuhakikisha lishe bora na matumizi sahihi ya chakula hicho.
Vyanzo vya Taarifa Hii:
1. Bunge la Tanzania: parliament.go.tz
2. Nukta Habari: nukta.co.tz
3. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS): nbs.go.tz
Kwa yeyote anayetaka uchambuzi zaidi wa takwimu hizi, tafadhali tembelea tovuti hizo kwa taarifa kamili.
Wadau,Karibuni tujadili na kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuboresha zaidi sekta ya kilimo na kuhakikisha lishe bora kwa Watanzania wote.
Inaongozea wapi?Bila Shinyanga kuwemo hiyo orodha ni fake! Kila mwaka Shinyanga inaongoza kuzalisha mpunga!
Hapa hapa Tanzania!Inaongozea wapi?
Yeah, ni kweli mahindi kwa wingi sana Kongwa, Mpwapwa na Kondoa!Pamoja na watu kupondea Dodoma ila ni Moja ya Mikoa muhimu Kwa uzalishaji hapa Tanzania na imeonesha wazi stori za watu waliokaririshwa ujinga wa vijiweni.
Ufuta ,Zabibu,mtama nkYeah, ni kweli mahindi kwa wingi sana Kongwa, Mpwapwa na Kondoa!
Nimeshtuka kuona Rukwa na Katavi hazimo hata katika 10, nikajiuliza yale mahindi na maharage yaani kumbe ni machache, wakati watu wanaamua hadi kuyapikia pombe!Hiyo ni list nilio itoa kwenye hizo website za serekali mkuu
Mkuu maharage ni Kagera mahindi ni RuvumaNimeshtuka kuona Rukwa na Katavi hazimo hata katika 10, nikajiuliza yale mahindi na maharage yaani kumbe ni machache, wakati watu wanaamua hadi kuyapikia pombe!
Lakini si umesema chakula kwa ujumla? Au ulitaja hiyo list kwa zao gani la chakula.Mkuu maharage ni Kagera mahindi ni Ruvuma
Leading regionsLakini si umesema chakula kwa ujumla? Au ulitaja hiyo list kwa zao gani la chakula.