Mikoa 10 Yenye Watu Maskini Zaidi Tanzania: Kagera namba 2, Dodoma namba 5. Nini Kinaiponza Mikoa Hii Maarufu?

Mikoa 10 Yenye Watu Maskini Zaidi Tanzania: Kagera namba 2, Dodoma namba 5. Nini Kinaiponza Mikoa Hii Maarufu?

Ukiona popotee CCM Ina nguvu jua haya
Makazi duni mfano Dodoma,pwani nk
Elimu duni mfano Tanga,tabora,mtwara,Lindi nk
Uchawi mfano Tanga,rukwa nk
Umasikini wa kipato nk kama takwimu zilivyo!!
Hiyo ni mikoa imekuwa chini ya CCM Kwa zaidi ya 60 years!!! Wabunge woooote CCM,madiwan woooote CCM,nk
 
Sio kwa ubaya nilikuwa sijawai fika kagera aisee nimeshangaaa sana. Kumbe huu mkoa ndio upo hivyo kiasi hiki nahisi huu ndio mkoa unaongoza kwa njaaa duniani.

Serikali inatakiwa kufungua huu mkoa kwa namna yeyote ile huku hakufai kufafuta maisha hata kidogo

Unaweza ukapauka sana.
 
First of all si mtu wa huko lakin nimewahi kufanya kazi huko at one time. Hiyo case ya kagera tu, mikoa mingine ina different factors

Is not an excuse it is a reality, jamii ambayo inajivunia mafanikio lakin mafanikio hayo wame invest kwenye mikoa mingine na si kwao… lazima nyumbani padode period
asilimia 80% wachaga wame invest nje ya mkoa wao ila kwao kuko poa kimzunguko wa kiuchumi.

sema jingine
 
A
Kwa Mujibu wa Uchambuzi kutoka Takwimu za Pato la Kila Mtu Kwa Kila mkoa Kwa bei za mwaka 2023,Mkoa wa Kagera na Dodoma imetajwa kama Mikoa maskini zaidi Tanzania ikishika namba 2 na namba 5 mtawalia.

Uchambuzi wa Takwimu zilizotolewa na NBS kwenye Chapisho lao la Tanzania in Figures 2023 unabainisha wastani wa kipato Cha Mtanzania Kwa mwaka (Per Capita Income) kuwa ni Shilingi Milioni 3.055.

Hata hivyo Kuna Mikoa ipatayo 15 ambayo Ina wastani wa kipato Cha mtu wa Chini kuliko Wastani wa Nchi wa Shilingi Milioni 3.

Wastani wa kipato Cha mtu inapatikana Kwa kuchukua Jumla ya Pato la Mkoa gawanya na idadi ya watu kwenye Mkoa husika. Kiufupi inakuwa ,
Regional Per Capita Income=Regional GDP/Population

Pamoja na kwamba Mikoa ipo 15 ila Mikoa 10 ndio Ina Hali mbaya zaidi ya kipato Kwa Watu wake na ndio nitaiweka kwenye orodha.

Mikoa hiyo nayoitambua kama Yenye watu Maskini Zaidi Tanzania kulingana na kipato ni ifuatayo; Figures are in Millions Tanzania Shillings)

1.Simiyu =1.54
2.Kagera =1.58
3.Singida =1.64
4.Pwani =1.81
5.Dodoma =1.89
6.Tabora =1.95
7.Kigoma =2.0
8.Katavi =2.1
9.Songwe =2.4
10.Rukwa =2.5

My Take
Mchawi ni idadi kubwa ya kuzaliana vs uwezo wa uzalishaji.

Pia soma Ni aibu kwa Dodoma na Kagera kuwa kwenye list ya mikoa 10 maskini zaidi Tanzania
View attachment 3060995

Soma zaidi hapa Mikoa 10 ya Tanzania Ambayo Wakazi Wake Wana Maendeleo na Kipato Kikubwa.

Angalizo
β€’Takwimu hizi sio rasmi Bali ni abstract tuu ya kutoa taswira ya Jumla ila sio Uchambuzi wa kina.

β€’Takwimu rasmi za marejeo ni zile zitakazotolewa na Mamlaka husika kama NBS,BoT,ESRF,FinScope nk.
Isee
 
Hatujuwi kama kuna ukwell lakini kwa dodoma nhnayoijuwa naona kama kuna uongo hapo. Ila siwezi bisha.
 
Back
Top Bottom