LGE2024 Mikoa 5 yavunja rekodi kujiandikisha uchaguzi wa TAMISEMI 2024 asema waziri Mohamed Mchengerwa

LGE2024 Mikoa 5 yavunja rekodi kujiandikisha uchaguzi wa TAMISEMI 2024 asema waziri Mohamed Mchengerwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Sababu za ripoti ya Sensa ya 2022 kutolewa December 2024, je nini TAMISEMI wamegundua ?​

October 19, 2024​

Ripoti ya Kina ya Matokeo ya Sensa na Malazi mwaka 2022 kutolewa Desemba 2024.​

img-20241019-wa001534602840008815300.jpg

Date: October 19, 2024Author: mtezamedia0
img-20241019-wa001534602840008815300.jpg

OFISI ya Taifa ya Takwimu(NBS) imesema kuwa wananchi wanasubiri ripoti ya kina kwa ajili ya kutumia katika maendeleo ambapo ifikapo Desemba 02, mwaka huu rasimu zote za ripoti za takwimu za sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022 zitakuwa zimekamilika.

Hayo ameyasema jijini Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Salum Kassim Ali kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali , Dk Albina Chuwa katika ufunguzi wa kikao kazi cha uandishi wa ripoti za kina zitokanazo na matokeo ya sensa ya watu na makazi mwaka 2022.

Amesema ya ripoti za kina zitokanazo na matokeo ya sensa ya watu na makazi mwaka 2022 na kuongeza kuwa kuzinduliwa rasmi awamu hii ya kwanza ya Uandishi wa Ripoti za Kina kunatokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

“Kutokana na miongozo ya Umoja wa Mataifa kuhusu ufanyaji wa Sensa ya Watu na Makazi, zoezi hili hukamilika tu pale ambapo uchambuzi wa taarifa zilizokusanywa zimechakatwa, zimechambuliwa na kuandaa ripoti za aina mbalimbali na ripoti hizo zitumike kikamilifu katika kufanya maamuzi mbalimbali yenye tija kuhusu mendeleo endelevu ya watu na makazi.

“Kwa msingi Serikali inaendelea na utekelezaji wa Awamu ya Tatu na ya mwisho ya zoezi la Sensa, katika awamu hii, Serikali imefanikisha kuandaa ripoti zote 24 za msingi ambazo zimeshazinduliwa rasmi,”amesema

Ali amesema serikali imeendelea kusambaza na kufanya mafunzo ya matumizi ya matokeo ya Sensa kwa viongozi na watendaji katika ngazi mbalimbali za utawala.

Ripoti ambazo zimeshakamilika zimebainisha viashiria vya msingi kwa jumla wake katika maeneo ya mgawanyo wa idadi ya watu katika ngazi mbalimbali za kiutawala, umri na jinsi, majimbo ya uchaguzi, takwimu za msingi za kidemografia, kijamii, kiuchumi na mazingira pamoja na takwimu za msingi za Sensa ya majengo.

Amesema Kitaalamu, ripoti hizo ni lazima ziandaliwe kwa kutoa picha ya hali ilivyo, maeneo yenye changamoto na fursa zilizopo kuiwezesha Serikali na wadau wengine kubuni na kutekeleza afua za kimakakati za kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii, kiuchumi na thibiti wa mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu ya wananchi wake.

“Napenda kutumia fursa hii kuwafahamisha wadau wetu wote kuwa, rasimu za ripoti 31 za takwimu za msingi za kidemografia, kijamii, kiuchumi na mazingira kwa mikoa yote nchini na ripoti ya Makadirio ya Idadi ya Watu kuanzia mwaka 2023 hadi 2050 zimekamilika.

Ali amesema rpoti hizi zitazindulia rasmi hivi karibuni kwa ajili ya matumizi kwa Umma.

Amesema baada ya kukamilisha uandishi wa ripoti za msingi za Sensa, Serikali imeelekeza nguvu zaidi katika uandishi
wa ripoti za kina za kisekta ambazo zimejikita katika kufanya chambuzi wa kina katika maeneo mahsusi.

Ali amesema maeneo yanayofanyiwa uchambuzi wa kina ni kati ya maeneo ya vipaumbe vya nchi ambayo yanahitaji takwimu za kina kufanya maamuzi sahihi zaidi ya kukuza na kuimarisha maendeleo ya watu.

Hata hivyo serikali imepanga kuandaa ripoti 15 za kina ambapo kazi hii itafanyika kwa awamu mbili.

“Katika awamu hii ya kwanza ambayo ndio imetukutanisha hapa leo, zitaandaliwa ripoti tano za kina katika maeneo ya Vizazi na Ndoa, Vifo na Afya , Hali ya Ulemavu, mienendo ya Idadi ya Watu na Elimu na kujua kusoma na kuandika.

Amesema lengo la kuandika ripoti hizi za kina za matokeo ya Sensa kama inavyopendekezwa na Umoja wa Mataifa ni kupata uelewa mpana zaidi wa hali ilivyo katika maeneo mahususi katika Nchi, kubaini mienendo, changamoto na fursa zilizopo kuwezesha viongozi na watendaji kuhuisha sera na mipango ya maendeleo inayoakisi hali halisi ya mahitaji ya wananchi.

Ripoti ya kina ya Mienendo ya Idadi ya Watu itawezesha kubaini mienendo ya idadi ya watu kwa umri na jinsi kati kipindi kimoja na kingine kwa kulinganisha na ukuaji wa uchumi na viashiria vingine kama vile hali ya uhifadhi wa mazingira na upatikanaji wa huduma za kijamii kwa ajili ya kuweka mikakati ya makusudi ya kuboresha maisha ya watu wote.

“Napenda kukuhakikishia kuwa tunao utaalamu wa kutosha ndani ya Nchi yetu kwa ajili ya kuifanya kazi hii muhimu ya kitaifa. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshghulikiwa Idadi ya Watu hapa Nchini, limeingia mkataba na Profesa Akim Mturi ambaye ni Mtanzania kuwa, awe Mshauri Mkuu wa Masuala ya Kitaalamu katika kufanikisha kazi hii,” amesema.

Alisema kazi hiyo ni kubwa na inahitaji utulivu, umakini, moyo wa kuijituma, kujitolea na uzalendo wa hali ya juu hivyo itatumia siku 14 kuchakata na kuandika rasimu za ripoti hizo.

Aidha, rasimu hizo zitawasilishwa katika Kamati za Sensa ngazi ya Taifa kwa ajili ya kuridhiwa uzinduzi wake.

Amesema Dkt.Albina aliagiza kazi hiyo ipewe nafasi ya kipekee katika kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa kwa kuwa inasubiriwa na Serikali na wadau kwa ajili ya kufanya maamuzi ya kimkakati yanayohusu maendeleo ya wananchi katika maeneo husika.

“Uandishi wa ripoti hizi za kina ni tofauti kidogo na ripoti zilizopita, hivyo natoa wito mzingatie yale yote ambayo Mshauri Mkuu wa Masuala ya Kitaalamu atakuwa anawaelekeza ili kufikia malengo liyojiwekea,” alisema.

Kwa upande wake, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Spika Mstaafu, Anne Makinda aliwataka kitumia utaalamu walionao kufanikisha kazi wanayoifanya ya uamdishi wa ripoti kwa viwango vya ubora na uwezo huo wanao.

“Ninazitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia takwimu za sensa kufanya maendeleo ya watu kwani kuendelea kuimarisha taarifa kunaipa tahamani uwekezaji unaofanywa na awrikali kushirikiana na wadau wa maendeleo, ” amesema
 

25 October 2024​

:FIRE: Taarifa za matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi zasaidia zoezi la uhakiki wa waathirika wa Maafa Hanang​

SERIKALI imetumia taarifa za matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022 kuthibitisha taarifa za makazi na kaya katika maeneo yaliyoathirika na maafa ya Maporomoko ya tope na mawe wilayani Hanang Mkoani Manyara.


c091cdbf220ff99dd3e3f0cd00b1ec2f


Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama .

Wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Ruvuma, iliyohusisha Kamati za Sensa na Wawakilishi wa Makundi Mbalimbali katika jamii tarehe 23 Disemba, 2023 katika ukumbi wa Njunde social hall – Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.


Waziri alisema, moja ya jukumu muhimu walilonalo ni kupata taarifa ya hali ya kaya, makazi na mali katika maeneo yaliyoathirika kabla ya maafa hayo.

“Hitaji hili lilipelekea timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya TAKWIMU kuja na taarifa ya kitaalamu iliyoambatana na picha za satellite ambazo zilionesha kwa uhakika hali ya kaya, makazi na mali zilizokuwepo katika maeneo hayo kwa idadi yake na maeneo zilizokuwepo,” alibainisha Mhe. Mhagama.


Aliongezea kuwa,licha ya kwamba wametumia vyanzo vingine pia kuthibitisha baadhi ya masuala katika maeneo hayo, lakini chanzo cha kwanza cha kuaminika kimekuwa ni matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwakumbusha kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Mwaka 2050 ambapo serikali imetoa fursa kwa wananchi kutoa maoni na mapendekezo.


”Niwasihi sana viongozi, watendaji na wananchi wote mshiriki katika zoezi hili ambalo ni muhimu kwa mustakabali mwema wa maendeleo ya nchi yetu, moja ya nyenzo muhimu zinazoweza kutuongoza kutoa maoni yetu ipasavyo historia ya taifa letu katika nyanja zote za siasa, uchumi, jamii pamoja na kuzingatia takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ikiwemo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022,”alifafanua.


Kwa upande wake Mwantumu Athumani Meneja Takwimu Mkoa wa Ruvuma akizungumza kwa niaba ya Mtwakwimu Mkuu wa serikali, alisema utoaji wa matokeo ya sensa ni tofauti na matukio mengine ya kitakwimu kwa kuwa wigo wa sensa ni mpana zaidi.


”Matokeo ya sensa hutolewa kwa awamu kulingana na ratiba ya utoaji na usambazaji wa matoke hayo ,” alisema


Ameongeza kusema kama kuna mdau anahitaji matokeo ya sensa, ambayo hayapo kwenye ripoti zetu kwa sasa anakaribishwa kuleta maombi yake kwenye ofisi Takwimu za mikoa.


Naye Mkazi wa Peramiho Bw. Tito Sowela alisema elimu ya sensa ya watu na makazi imeongeza uelewa mpana wa wananchi hasa juu ya taarifa zinazokusanywa na namna zinavyoweza kusaidia serikali katika kupanga miradi ya maendeleo kwa wananchi

Source : PMO | Habari
 
Back
Top Bottom