Mikoa au miji yenye mzunguko mzuri wa pesa

kahata

Member
Joined
Jan 17, 2021
Posts
88
Reaction score
53
Msaada nahitaji kuanza biashara ya nguo, viatu pochi na mikoba, ni mikoa na miji ipi yenye mzunguko mzuri wa pesa na inafaa kwa biashara ukiondoa daresalaam?

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mahali sahihi zaidi ukishaanzisha biashara itaendelea kama ukiwa na usimamizi mzuri, Kuhusu mzunguko wa pesa hii inategemea na mtaji wako, huwezi kusema unataka ufanye mauzo ya laki 5/6 /7 hadi 1milioni wakati mtaji wako upo chini ya milioni kumi huo ni UWONGO.

Mtaji wako ukiwa mnono mauzo nayo yatakua hivyo hivyo.

Location- Biashara yoyote inahitaji Centa mahali panapofikika kirahisi.
 
Njoo mwanza , utanishukuru
 
Kwa ushauri wangu fanyia tu Dar....nimezunguka mikoa mingi ya TZ karibu yote ni migumu kibiashara
Kila mkoa una aina za biashara zake. Kwa mfano Ruvuma dili na pembejeo za kilimo, vifaa vya ujenzi, Pharmacy zinatoa pia.

Kutoboa biashara nyingine inahitaji ubunifu na uvumilivu sana.

Kwa hiyo mimi huwa siamini kuna mikoa migumu kibiashara. Shida unaenda kufanya biashara gani.

Ni sawa ukafungue duka la kisasa nguo Kisesa ndani ndani huko halafu utegemee matokeo makubwa. No way.
 
Kwa ushauri wangu fanyia tu Dar....nimezunguka mikoa mingi ya TZ karibu yote ni migumu kibiashara
Huu ndio ukweli angalau kidogo mwanza wanajitahidi ila hii dar ni kubwa ni kutafuta ka eneo unajiposition basi unaanza kulipa hela ya ulinzi
 
Dar Ni sehemu sahihi Sana hakuna masuala ya ukabila pia idadi kubwa ya wtu hupenda vitu vya fashion hivyo Ni rahisi kupata fedha tofauti na mikoani wengi wajikita siku za sikukuu au matukioa Kama harusi bidhaa zako zitalala lakin Dar watu wanakwenda na wakati pia wanamashino pia watu wengi wa Dar wanavipato vya uhakika
 
Back
Top Bottom