Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,604
- 5,583
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna yeyote aliyenyimwa kupiga kura kama unavyofikiri wewe.Unapojadili maswala magumu sana ya nchi jaribu kuwa katikati bila kuegemea popote ili upate uhalisia wa mambo.Nyaisonga na pengo wanayajua hayo. Kwamba waumini wao wamenyimwa haki ya kuchagua wawakilishi wawatakao?
Tafsiri ya kupita bila kupingwa umewahiona wapi duniani?Hakuna kitu kama hicho watu wanayo haki ya kuwachagua wawatakao wagombea washindanishwe ili watu wachague.Kupita bila kupingwa ni sawa na viti maalumu pia ni sawa na zama za giza pale watu walipolazimishwa wachague kivuli au sura ya mtuHakuna yeyote aliyenyimwa kupiga kura kama unavyofikiri wewe.Unapojadili maswala magumu sana ya nchi jaribu kuwa katikati bila kuegemea popote ili upate uhalisia wa mambo.
Kila anayestahili kupiga kura sio mtoto mdogo kwa mujibu na kanuni za uchaguzi.Kwa hivyo sioni kama unaweza kumshawishi au kumchagulia apige au asipige kura kumchagua mwakilishi au kiongozi wake kwa sababu Watanzania sio wajinga.
Na kama kuna dalili hizo,tusubiri huo uchaguzi.
Mimi siamini kuwa waumini wamenyimwa haki ya kwenda kuchagua wawakilishi wao nasema hivi kwa sababu hakuna ushahidi wa walionyimwa haki hiyo.Pili uchaguzi haujafanyika,wao hizo data za waumini watu wazima kukatazwa kupiga kura wamezipata wapi.Najua baada ya kura kuhesabiwa ndo unaweza kuzungumza au kusema mtoa post aliyoyasema na asiwahusishe viongozi kwenye maji yaliyokwisha mwagika kwani yakishamwagika yamemwagika huwezi kuyasomba tena. wao Kama wameshapiga kura kimya kimya hizo data Waziweka hapa tuzione.Na nawashauri waachane na viongozi wa dini za watu.
Napenda kushangaa sana kwa sababu,siku zote sakata hili likiendelea viongozi hawa wa dini hawakuhusishwa popote.Mambo yamekuwa magumu Watanzania wako njia panda viongozi wa dini wanahusishwa kiaina aina kwa kudanganywa kuwa kuna watu wanashawishi waumini wao.Leo hii wanawageuzia kibao waumini kuwa wanashawishiwa.Napenda kusema kuwa hakuna wa kumshawishi muumini..
Swala liko hivi kila mwenye macho ameona hii drama inavyopelekwa.Hata mimi niliiona.Kama ukishaona na kutambua mwisho wa drama,mwenye akili huendelea na shughuli zake na kuwaacha wenye drama yao waendelee.
Watanzania wengi wameiona na sioni kama kuna ushawishi wowote unaotolewa kwa watu wazima hawa.Bali drama mwisho umeoneka wakaamua labda kukaa pembeni.
Hata hivyo kama mtu hakujiandikisha hana sifa ya kupiga kura na hahitaji ushawishi wowote,hivyo tusidanganyane bali tuwe wakweli ili Tanzania ipone.
Ushindi wa kishindo tayari katika mikoa 3