Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Bashungwa ametoa maagizo hayo leo, Februari 17, 2025, alipotembelea Maabara ya Uchunguzi wa Makosa ya Kimtandao katika Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai, jijini Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kila robo ya mwaka inaonesha kuwa mikoa ya Rukwa, Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam inaongoza kwa vitendo vya utapeli wa mtandaoni, huku maeneo hayo yakiendelea kujirudia katika ripoti hizo.
“Katika kipindi cha miaka miwili, matukio ya uhalifu mtandaoni yameongezeka katika mikoa hii, ambapo Morogoro, hususan eneo la Ifakara, limeonekana kuwa kinara,” amesema Bashungwa.
Bashungwa amelitaka Jeshi la Polisi kukomesha mtandao mpana wa wahalifu wa mtandaoni, ambao hushirikiana kati ya mkoa mmoja na mwingine katika kuratibu vitendo vya wizi na utapeli.