Mikopo hii itaniuwa sasa

kirisha

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2017
Posts
573
Reaction score
663
Jamani naombeni ushauri nimekopa kwa watu binafsi na tasisi za kifedha paka sasa na Deni langu limepanda sana na kufika 7700000 milioni Saba na laki Saba

Mzigo dukani kwangu upo ila siyo mkubwa kawaida. Sasa nimemuomba rafiki yangu ushauri jinsi ya kupata pesa niweke mzigo ili nizungushe kipindi hiki cha sikukuu.

Kanishauri niende kwenye tasisi moja nikope milioni moja niweke mzigo dukani kisha nirejeshe na kupunguza madeni.

Nimewaza na hali yangu ya madeni nikiongeza tena madeni nitatoboa kweli!

Najua huku Jamiiforums Kuna watu waliopitia shida Kama hizi zangu, naombeni ushauri nichukue hiyo milioni au nikomae na huu mzigo uliopo dukani!
 
nikomae na huu mzigo uliopo dukani
Kama mzigo unao na msimu wa sikukuu unakaribia, logic ya kukopa ni Nini? Au huenda sijaelewa! Si uendelee na mzigo uliopo hata kama ni Mdogo?! Kuliko kujiingiza kwenye madeni zaidi? Hili nalo ni la kushauriwa? Au Kuna taarifa hujaitoa?
 
Komaa na huo mzigo. Madeni yakishakua mengi kuliko mtaji ujue teyari ni anguko hilo. Kubali kupoteza dhamana zako na wewe kujipanga kuanza upya.
 
Kama mzigo unao na msimu wa sikukuu unakaribia, logic ya kukopa ni Nini? Au huenda sijaelewa! Si uendelee na mzigo uliopo hata kama ni Mdogo?! Kuliko kujiingiza kwenye madeni zaidi? Hili nalo ni la kushauriwa? Au Kuna taarifa hujaitoa?
Mzigo upo kiasi ila mali iliyopo nyingi ni ile ambayo kuenda kwake ni mdogo mdogo sana. Sasa nilishauriwa nichukue mkopo niweke na mali zinazokwenda kwa kasi nipige msimu huu wa sikukuu niweze kupunguza madeni. Sasa Mimi nimesita kidogo kwasababu majukumu ni mengi yanayonikabili na ya lazima madeni yamekuwa makubwa.

Ndio naomba ushauri nichukue hiyo milioni niongeze mali dukani au nikomae tu
 
Komaa na huo mzigo. Madeni yakishakua mengi kuliko mtaji ujue teyari ni anguko ilo. Kubali kupoteza dhamana zako na wewe kujipanga kuanza upya
Madeni ni makubwa kuliko mtaji paka Sasa hivi
 
Madeni ni makubwa kuliko mtaji paka Sasa hivi

Usiongeze deni. Kama huko na assets zako uza ili uongezee mtaji kwenye mzigo unaotembea.

Au huo mzigo usiotembea uza katika faida ndogo au uza pasipo faida ili uweke hiyo bidhaa unayoamini wewe inatembea.

Unaweza pia uza kwa hasara ila hasara isiwe kubwa. Iwe inakaribiana na ongezeko la riba kwenye mkopo unaochukua. Kuliko kuwa na mkopo bora uwe na pesa yako mwenyewe ya kuanzia upambanaji.

Mfano unataka kopa 1M kwa malipo pamoja na riba 1.2M.

Vyema ukauza mzigo wako usiotembea ukukate walau hasara ya 100,000 ila isiyozidi au kukaribia riba
 
Asante sana kwa mawazo mazuri
 
Ongezea madeni mwanangu.. kwani shi ngapi mzee baba. Wee ongeza deni tu halafu nenda bar ongeza bia. Alaah..
 
Hivi ukitoa ufafanuzi wa biashara unayofanya ukapata ushauri-ni vibaya au business yako ni unique sana hapa Tanzania?
 
"Mzigo" ni relative term....

Na huo mzigo unaoisemea uusukume kipindi cha sikukuu ni vyakula, mavazi au mapambo au vifaa vya ujenzi?
 
Wafanya biashara sometimes tunafeli kitu kimoja tu!, Ni kujaza duka ili kupendezesha duka na bidhaa ambazo hazina mzunguko! Mkuu usifanye biashara unavyotaka wewe bali fanya biashara inavyotaka biashara kama unauza nguo, saa, mikanda na ukagundua saa ndio zina mzunguko weka nguvu zako huko.
 
Kukopa ni roho, hii roho ikikuingia lazima ufilisike. Hii roho inaitwa Behemoth, haishibi. Ina fanyakazi ya kufilisi, roho hii na Dagon ndizo zinazoachilia madeni. Leviathan ndiye roho aliyetumwa⁵ kumfilisi Ayubu.

Hebu jaribu kupambana rohoni kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…