Jamani naombeni ushauri nimekopa kwa watu binafsi na tasisi za kifedha paka sasa na Deni langu limepanda sana na kufika 7700000 milioni Saba na laki Saba
Mzigo dukani kwangu upo ila siyo mkubwa kwaida Sasa nimemuomba rafiki yangu ushauri jinsi ya kupata pesa niweke mzigo ili nizungushe kipindi hiki cha sikukuu
Kanishauri niende kwenye tasisi moja nikupe milioni moja niweke mzigo dukani kisha nirejeshe na kupunguza madeni
Nimewaza na hali yangu ya madeni nikiongeza tena madeni nitatoboa kweli
Najua huku jamii forum Kuna watu waliopitia shida Kama hizi zangu naombeni ushauri nichukuwe hiyo milioni au nikomae na huu mzigo uliopo dukani
Huu ndo ushauri wangu, you are going down and you're going total down, usitengeneze mashimo mapya ukitegemea utainuka, usikope tena.
Cha kufanya:
1. Deni haliui, linaleta tu aibu na psychological torture.
2. Usikope mahali au kutumaini utalipa hilo deni.
3. Kama bond sio nyumba au kiwanja, wewe jitahidi tu kwenye biashara, ukishindwa basi.
4. Jiandae kupoteza kila kitu na kuanza upya.
Note:
1. Hakuna mtu mwenye mamlaka yeyote ya kukunyang'anya kitu bila ruhusa ya mahakama, kwahiyo usitishwe na mtu.
2. Kama rehani ni nyumba au kiwanja, jitahidi uuze haraka ulipe deni angalau ubakiwe na hela, mahakama ikikubali ufilisiwe hutapata kitu.
3. Usijali, usijiue, haya huwa yanakuja na kupita. Yanaaibisha na mwishowe huisha, watu kibao wanadaiwa na wanashindwa kulipa.
4. Kama una mke/mme muweke wazi kuepuka depressions, na kama hujaoa au kuolewa, elezea wazazi wako au wakuu wa dini angalau upate faraja.
5. Maisha ni vita, pigana, umeanguka hapa, ila utaondoka na uzoefu, rekebisha na endelea kupambana tena tena.
6. Jaribu kuwa na mitizamo yako na sababu za kukopa sio kushauriwa na watu, biashara ni yako, sikiliza moyo wako.