Mikopo isiyo na Riba kwa watumishi wa umma

Mikopo isiyo na Riba kwa watumishi wa umma

Ze Heby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
5,926
Reaction score
6,742
Habari ndugu watumishi wa sasa na wale watarajiwa

Serikali huwa inatenga kiasi cha pesa kwa ajili ya kuwakopesha watumishi wake. Mikopo hii haina riba kabisa (ukiacha gharama kidogo sana za kuprocess). Lengo la mikopo hii ni kuwasaidia watumishi kupata fedha za kujenga nyumba, kununua usafiri, fenicha nk.

Mikopo hii ikitoka hapo kwenu, CHUKUA. Yes, chukua tu, haina riba, huna cha kupoteza, we chukua tena hakikisha unachukua maximum limit kutegemea na mshahara wako.

Lakini sasa ukishachukua, usiende kujenga nyumba, wala usiende kuanzisha biashara mpya unless kama una biashara ambayo iko operational tayari na inaingiza faida. Badala yake, nenda kaiwekeze kwenye maeneo yenye hatari ndogo, itakua inakupa kipato kila mwezi ambao ni almost sawa na makato unayokatwa.

Kama una risk appetite kubwa, unaweza kuwekeza kwenye hisa za makampuni yanayofanya vizuri na ukifanya analysis vizuri, unaweza kupata almost 100% capital gain in a year kama ilivyotokea kwa CRDB etc.

Zingatia kuwa, mkopo huu ni tunu adhimu sana kwa sababu HAUNA RIBA kwa hiyo unarudisha ulichopewa, utumie mkopo huu kutengeneza pesa kwa njia salama ili uweze kujikwamua kimaisha.

Salaam.​
 

Attachments

Umesoma vizuri tarehe za hayo matangazo?
Hii ni mifano ya matangazo ya miaka iliyopita kwa halmashauri chache. Hizi pesa huwa zinakuja kila halmashauri mara kwa mara na matangazo huwa yanatolewa kwenye website ya halmashauri husika​
 
Hii ni mifano ya matangazo ya miaka iliyopita kwa halmashauri chache. Hizi pesa huwa zinakuja kila halmashauri
Hizi pesa huwa wanagawana jamaa wa utumishi kwanza zikibaki ndio wanapewa wengine.

Utumishi wana roho zao za kipekee.
 
Riba zinayo asilimia 02 na wanakata riba yao kabisa kinachobaki ndo wanakupa tatizo wanatoa hela ndogo sana huwezi pata zaidi ya milioni tano
 
Riba zinayo asilimia 02 na wanakata riba yao kabisa kinachobaki ndo wanakupa tatizo wanatoa hela ndogo sana huwezi pata zaidi ya milioni tano

Hiyo sio riba, inaitwa processing fee na huwa ni one time. Kiasi cha mkopo inaweza kufika hata 20 M kwa mtumishi afisa wa kawaida
 
Hizi pesa huwa wanagawana jamaa wa utumishi kwanza zikibaki ndio wanapewa wengine.

Utumishi wana roho zao za kipekee.

Hawawezi kugawana sababu zinakuwa disbursed directly kutoka hazina maana zinaombwa kwenye mfumo moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom