Mikopo isiyoenda katika shughuli za kiuchumi ina maana gani kwa taifa letu?

Mikopo isiyoenda katika shughuli za kiuchumi ina maana gani kwa taifa letu?

Am focused

Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
41
Reaction score
173
Moja kwa moja niende kwenye maada kama kichwa cha habari kinavyosema

Kumekuwa na sintofahamu juu ya kauli iliyotolewa na mheshimiwa spika, bwana Job Ndugai hivi karibuni na hata yeye mwenyewe ameamua kuikana kauli yake baada ya mashinikizo kadhaa kutoka kwa watu na viongozi mbali mbali

Tusijadili kwanza kauli ya mheshimiwa spika ila ningeomba nitanabaishe kwa upande wangu kwamba mheshimiwa alikuwa sahihi kutoa ile kauli lakini sababu watanzania wengi hawako upande wake hasa ukizingtia matendo yake kipindi cha magufuli na baadhi ya viongozi ambao wanalinda matumbo yao kupitia mikopo hiyo.

Tujadili maada hii mikopo ya matrilioni ambayo haiendi kutumika katika shughuli za kiuchumi na badala yake zinaenda kujenga vyoo, madarasa na sehemu zingine zisizo na shughuli za kiuchumi inarudishwa kwa njia gani?

Kwanini hii mikopo isitumike sehemu “potential” tu ambapo kunakuwa na ulazima katika miradi mbali mbali ambayo itajiendesha kurejesha mikopo hiyo?

Kuna “agenda” gani juu ya hii mikopo ambayo haiendi katika uzalishaji?

Msitumie mihemko kujibu hayo maswali sababu najua kuna baadhi ya watu humu wananufaika na mifumo iliyopo hivyo watakuja na hoja nyepesi

Pia elimu za viongozi wengi ni ndogo sana ambazo zinawafanya wasiweze kufikiria juu ya haya mambo

Viongozi wengi hawana uzalendo juu ya hili taifa, kila mtu anataka kujinufaisha kwa wakati wake na hivyo watanzania wengi kukosa maendeleo na mwelekeo kwa ujumla.

Tuweke siasa pembeni tujadili hoja tajwa!

👆🏾
 
Mi kinachonipa hasira sio kukopa ila hzo hela haziendi sehemu husika watu wanatafuna tu hawajali.
 
Back
Top Bottom