Mikopo ‘kausha damu’ yatajwa kusambaratisha familia, wanandoa

Mikopo ‘kausha damu’ yatajwa kusambaratisha familia, wanandoa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Chama cha ACT-Wazalendo kimeiomba Serikali kupitia mfumo mzima wa ukopeshaji unaotekelezwa na taasisi zisizo za kiserikali nchini kwa kuwa wananyinywa na kuhatarisha maisha ya wanawake.

Kimetolea mfano wa mikopo inayojulikana kausha damu kuwa licha ya kuwasumbua wanawake pia imevunja ndoa nyingi.

Ombi hilo limetolewa leo jumanne jioni na Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Tanzania Bars,Doroth Samu wakati wa kongamano la kitaifa la wanawake lililofanyika jijini hapa.

Amesema kutokana na hali ngumu ya maisha wanawake wengi nameingia katika majukumu la kusaidiana na waume zao katika kulea familia hivyo wanalazimika kukopa kwa mategemeo ya kuendesha maisha na maendeleo kwa ujumla.

Amesema tofauti na matarajio yao wamejikuta wakifanya kazi za kuzitajirisha taasisi zinazowakopesha kwa sababu zinatoza riba kubwa isiyolipika kwa njia za rahisi.

"Wanawake ndiyo waathirika wakubwa wa mikopo hiyo kwa sababu wanalazimika kujiunga na mikopo mingi ili waweze kulipa...lakini wanajikuta wakiingia katika migogoro ya ndoa na wengine wanaamua kukatisha maisha yao kwa sababu ya msongo wa mawazo ya madeni," alisema Doroth.

Amesema njia ya kuwasaidia wanawake nchini ni kufanyia marekebisho mfumo mzima wa riba katika mikopo ya taasisi binafsi ili isiweze kuwanyonya wakopaji.

MWANANCHI
 
Famasiala na kausha damu😀😀😀
 
Hii mikopo kausha damu ni ishara kubwa kuwepo kwa umasikini na ufukara mkubwa katika jamii
 
Nimeshangaa sana kuna watu na hivyo vitaasisi vyao, eti wanawakopesha wanawake tu! Maana wanajua fika wengi wao ni waoga. Yaani mwanamke akikopa labda laki 1, basi kila siku anatakiwa kutuma 4500!
Akikosa kutuma, atafokewa kama mtoto mdogo, na atalipishwa na faini juu!!

Nadhani serikali inatakiwa kuonheza juhudi ya kuwahamasisha akina mama kujiunga katika vikundi, halafuikawakopesha mikopo yenye riba nafuu au ile mikopo isiyo na riba, ili kujikwamua kiuchumi.
 
Back
Top Bottom