Mikopo kwa walimu, NMB vs CRDB

Kiongozi hiz taarifa zako si sahihi kabsa. Mikopo ya watumishi kwa crdb ni 18%(pamoja na bima). Processing fee ni 1.5% ya total loan. Hakuna garama ya pass. Pass ni kwa ajili ya mikopo ya kilimo. Nmb ni sahih riba ya watumishi wa kawaida ni 20% wanajeshi ni something like 13% hivi na madiwani ni 17. Madiwani ni 16 kwa crdb. Pia Crdb muda wa marejesho ni hadi miaka 6. Kwa nmb sina hakika ila last time nilipofuatilia ilikuwa ni 5 yrs.
 
Daaa!hatari ila bank ya posta ndio hawafai kabisa naona riba yao ni asilimia 90 kwamana laki na 86 kwa miaka 5 wanakupa million 5 na laki 8 hebu angalia riba hiyo
 
crdb mkuu hutajuta ukimaliza process zote soon tu hawabagui wateja ila jipu nmb hapana pia nmb riba yao imezidi kidoogo
 
CRDB wako vizuri sana katika hili Muhimu ww kama mkopaji umalize process ndani ya muda mwafaka af mikopo sikuizi inachukua siku tano za kazi hivo kama unahitaji mkopo mkubwa na wenye tija huto juta kuchukua Mkopo CRDB na kitu cha msingi riba ya CRDB inavochukuliwa ni tofauti kidogo na Bank nyingine kwao Riba inaenda ikipungia
 
Sasa hivi wiki ya tatu crdb mshikaji wangu hajawekewa
 
Nimependa hii mada mleta mada nakutunuku udaktari WA miezi mitatu . Ikiisha ubaki vile vile ulivokua
 
Acha kupotosha mkuu..
Riba ya CRDB kwa personal loans zote ni 18%(ikihusisha na 1% ya bima ndani yake) wala sio 24% kama unavodai.
Ila mkopo wowote wa Crdb kama ilivyo kwa benki nyingine lzm kuwepo na ada.
●Kwa CRDB iko ni 1.1% ya mkopo ni Loan application fee na minimum ni 110,000
●0.55% ya mkopo ni Loan processing fee na minimum ni 55,000
Kwa mfano mikopo yote inayoanzia 5,000,000 na kushuka had 1,500,000 ada yake ni 165,000 tu(minimum threshold) ambayo ni one-time fee.
●Na kuanzia mwezi Disemba mwaka CRDB inakopesha hadi miaka 6.
Huu ndo ukweli na huhitaji kujua mimi ni nani CRDB ili uniamini
 
Mkuu, nimependa mno ufafanuzi wako. Je kuna uataraibu gani wa kufuata kwa mwalimu kuomba mkopo CRDB? provided mshahara wake unapitia NMB?
 
Mkuu, nimependa mno ufafanuzi wako. Je kuna uataraibu gani wa kufuata kwa mwalimu kuomba mkopo CRDB? provided mshahara wake unapitia NMB?
Utaratibu ni rahisi tu
●Barua ya kuajiriwa
●Barua ya kuthibitishwa kazini
●Salary slip za miezi 3 ya karibuni
●Picha(passport size) mbili
●Barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri
●Barua yako ya kuomba mkopo(ipitie kwa mkuu wa kituo chakp cha kazi)
●Bank statement ya angalau miez mitatu ya unakopitia mshahara wako
●Kitambulisho chako,e.g cha kazi,cha kupira kura etc
Na lazima uwe na akaunti katika benki ya CRDB ambako mkopo wako utawekwa huko .
Ni hivo tu
 
Kama mie mshahara wangu ni 525000 kwa mfano ntakua naeza kopeshwa sh ngap??
 
Kama mie mshahara wangu ni 525000 kwa mfano ntakua naeza kopeshwa sh ngap??
Natakiwa nijue Gross pay(basic salary ongeza na allowances zako ambazo ni static) nijue na take home...
Halafu pia unambie unataka kukopa kwa muda gani?
 
mkuu barua ya sijui ya ajira/ kuthibitishwa kazini vip hamuhitaji kwa hiyo
 
Kwa sasa Tanzania, benki ni NMB PLC kwa mahitaji yako yote kwa kukopa na huduma zote za kibenki.
 
Kwa sasa Tanzania, benki ni NMB PLC kwa mahitaji yako yote kwa kukopa na huduma zote za kibenki.

NMB wasumbufu Sana. Maloan officer wanaringa, wasumbufu na wanapenda kuachiwa hela kidogo. Watabakia na wafanyakaz wachache Sana kwasababu hawataki kubadilika kuendana na ushindani wa kibiashara. Mtu unakopa ila unanyanyaswa unadhan unaomba msaada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…