Kidaya
Senior Member
- Dec 20, 2011
- 108
- 95
Michezo, Sanaa na utamaduni ni ajira, burudani, biashara na utambulisho wa Taifa. Sekta ya michezo, sanaa na utamaduni ni sekta muhimu kiuchumi katika nchi zilizoendelea kwa mfano nchini Uingereza, sekta ya michezo inakadiriwa kuchangia kiasi cha Tsh. trilioni 110.9 kwa mwaka kwenye pato la Taifa (takwimu za Sport England). Hali ni tofauti sana kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania ambapo kwa mwaka 2022 sekta ya michezo ilichangia kiasi cha Tsh bilioni 1.7 tuu kwenye pato la Taifa (Ofisi ya Waziri Mkuu). Changamoto kubwa zinazoikabili sekta ya michezo nchini Tanzania ni pamoja na ukosefu wa fedha za kutosha kugharamia wanamichezo na timu za michezo, uhaba wa miundombinu bora, ukosefu wa mafunzo endelevu na uhaba wa walimu wa michezo na sanaa.
Kutoa mikopo kwa wanamichezo na wasanii nchini Tanzania kutaboresha sekta ya michezo kwa kutoa rasilimali fedha zinazohitajika kukuza na kuendeleza vipaji vya wanamichezo na wasanii.

Faida za mikopo kwa wanamichezo
• Mikopo itawasaidia wanamichezo kupata mafunzo ya hali ya juu, vifaa vya kisasa, kumudu vituo bora vya mafunzo, na kuajiri makocha/walimu mahiri, hali itakayoboresha utendaji wao katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, na kuinua hadhi ya michezo ya Tanzania duniani.
• Mikopo itasaidia wanamichezo kumudu gharama za kushiriki katika mashindano ya kimataifa hasa za usafiri, malazi, na ada za mashindano, ili kuwawezesha kupata uzoefu, ujuzi na kutambulika kimataifa hali itakayosaidia kuvutia wawekezaji, wadhamini, na ushirikiano.
• Wanamichezo wenye mafanikio wanazalisha kipato kikubwa kutoka mishahara, matangazo, udhamini, na zawadi za fedha. Kipato hiki wanawekeza katika uchumi wa ndani kupitia njia mbalimbali kumiliki mali zisizohamishika, na kuanzisha biashara ambazo huchochea ukuaji wa kiuchumi na kunufaisha jamii kwa ujumla.
• Mafanikio ya wanamichezo yanaweza kuvutia wadau mbalimbali kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo ili kuzalisha wanamichezo wengi zaidi, kama vile uwekezaji wa viwanja, vituo vya mafunzo, na akademi za michezo, hivyo kuimarisha zaidi uchumi wa michezo.
• Mikopo itawapa wanamichezo mitaji ya kuandaa matamasha/mashindano, kuanzisha biashara, akademi za michezo, vituo vya mazoezi, na chapa (label) za kazi au biashara. Miradi hii inawapa wanamichezo njia za kukuza vipaji, kuongeza kipato, kutoa fursa za ajira na kuchangia uchumi.
• Wanamichezo huwa watu maarufu na hutumika kama mifano, kuhamasisha vijana kufuata ndoto zao na kufanya kazi kwa bidii kufikia malengo yao. Kwa kutoa mikopo kusaidia taaluma zao, mifano hii inaweza kuendelea kufanikiwa na kuathiri vyema vijana kushiriki katika michezo kama ajira.
• Taaluma za michezo zinaweza kuwa fupi kutokana na mahitaji ya kimwili ya michezo. Mikopo itasaidia wanamichezo kujiandaa kwa maisha baada ya michezo kwa kufadhili elimu na ujuzi unaohitajika kwa kazi katika mafunzo ya ukocha, usimamizi wa michezo, vyombo vya habari, mafunzo ya uelewa wa kifedha au maeneo mengine hivyo kudumisha usalama wao wa kifedha na mchango wao endelevu kwa jamii.
• Kutoa mikopo mahsusi kwa wanamichezo wa kike inaweza kusaidia kuhakikisha wanayo fursa sawa za kufanikiwa katika michezo. Hii inakuza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanamichezo wakike, kuchangia maendeleo mapana ya kijamii.

Utaratibu wa mikopo kwa wanamichezo na wasanii
Kwa miaka mingi sasa tumekuwa na utarataibu wa wazi wa wanafunzi na wanataalluma mbalimbali kuomba na kupata mikopo na ufadhili wa masomo yao. Hali ni tofauti kwa wanamichezo ambao mara nyingi wanapambana wenyewe kufikia malengo na mafanikio yao. Wizara ya michezo iwe na kitengo cha mikopo ya wanamichezo kwa angalau jumla ya wanamichezo 10 kwa mwaka kwa makundi yafuatayo;
• Wanamichezo wanaochipukia ili kuwawezesha kupata mafunzo stahiki katika nchi zinazoweza kuendeleza vipaji vyao. Mfano Messi anaetajwa kuwa mchezaji bora wa dunia wa muda wote, alipelekwa nchini Hispania kuendeleza kipaji chake. Inawezekana na Tanzania wakawepo akina Messi wengi wa badae wanaokwamishwa na hali zao za kiuchumi.
• Wanamichezo wanaohitajika kwenda kushiriki mashindano/matamasha kwenye miji mikubwa mbali na makazi yao. Biashara kubwa ya michezo ipo zaidi kwenye miji mikubwa, kuna wanamichezo/wasanii wa mikoani wanashindwa kufika mijini kuonesha uwezo wao.
• Wanamichezo wanaohitajka kwenda kushiriki mashindano/matamasha nje ya nchi ili kuonekana na kuwaongezea nafasi za fursa zaidi.
• Wanamichezo wanaohitaji kuandaa matamasha na mashindano mbalimbali ili kutoa nafasi kwa wanamichezo kuonekana zaidi na kujipatia kipato.
• Wanamichezo wanaotaka kufanya uwekezaji wa kimichezo kama kufungua vituo vya michezo, kujenga miundombinu za michezo n.k.
• Wanamichezo wanaotaka kujiendeleza kitaaluma kama kusomea ukocha/ ualimu wa michezo, uamuzi wa michezo n.k.

Urejeshaji wa mikopo ya wanamichezo na wasanii
Wanamichezo na wasanii wana uwezo mkubwa wa kurudisha mikopo mapema zaidi kuliko wataaaluma wengine kutokana na sekta ya michezo na sanaa kuwa na mishahara mikubwa sana na mapato ya ziada yanayotokana na matangazo na udhamini. Mfano mwanamichezo au msanii mmoja anaweza kulipwa Tsh. Milioni 100 kwa mwezi au kwa tukio/tamasha tofauti na wanataaluma wengi ambao mapato yao yana wastani wa Tsh. Milioni moja kwa mwezi. Mamlaka husika zitaingia mikataba ya urejeshaji wa mikopo hii kwa kutegemea asilimia za jumla ya mapato anayopata mwanamichezo. Kwakuwa wanamichezo huwa watu maarufu ni rahisi zaidi kuwafuatilia kurejesha mikopo yao kuliko wanataaluma ambao wengi hawajulikani walipo baada ya kumaliza vyuo, hivyo mikopo mingi kutorudishwa kwa wakati au kutorudishwa kabisa.
Kutoa mikopo kwa wanamichezo na wasanii nchini ni fursa kubwa ya kuboresha sekta ya michezo, kutoa fursa za ajira, na ukuaji wa kiuchumi. Fursa hii itawasaidia kuweza kufikia uwezo wao kamili, kufikia mafanikio na kuhamasisha wengine. Uwekezaji huu katika michezo unaweza kuzalisha faida mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuboresha afya, kujenga uzalendo na fahari ya nchi, na kuitangaza nchi yetu kimataifa, kuboresha taaluma za wanamichezo binafsi, kukuza michezo katika ngazi za msingi, na kutoa faida za kiuchumi kwa wanamichezo na taifa. Mikopo ya kifedha, mifumo ya ufadhili, na ushirikiano wa kimkakati ni muhimu katika kuongeza faida hizi na kuhakikisha uendelevu na ukuaji wa sekta ya michezo nchini Tanzania.
Tahadhari: Katika makala hii neno mwanamichezo linajumuisha watu wote wanaojishughulisha na aina fulani ya mchezo, sanaa au utamaduni kwa lengo la kujipatia kipato. Shughuli hizi ni kama uchezaji wa mipira aina zote, ndondi, usanii wa muziki, uigizaji na michezo ya kiutamaduni.

Upvote
12