ndunajr
Senior Member
- Apr 28, 2015
- 184
- 210
Najaribu kufikiri Mimi mswahili. Hivi kwa Nini Afrika hutuwezi kutumia akili nyingi kuwawezesha watu wetu.
Ishu ya mikopo hasa kwa watu walio na ajira, nimeona wengi pamoja na kuajiriwa kwao lakini hawawezi kudhaminika kwenye mabenki. Ofisi nyingi zinashindwa kudhamini wafanyakazi wake kupata mikopo kutoka kwenye mabenki mbalimbali.
Mimi kama mtanzania ambaye pia ni mhanga, natamani siku Moja pawepo na kiongozi mwenye akili nyingi aunganishe mabenki na mifuko ya jamii kama NSSF,PSSSF n.k, yani kusema kwamba mabenki yaingie kwenye makubaliano na mifuko ya Jamii ili mtu yoyote aliyeajiriwa aweze kudhaminika na mfuko wake wa jamii. Mfano, Nina milioni 15 NSSF ingeweza kunikwamua kama dhamana na benki wakanipa mkopo labda milioni tano pengine hata ningeweza kiwekeza kwenye biashara flani ambayo make wangu asimamie ili iingize kipato mbadala kwenye familia, halafu sasa niwe nalipa kwa mshahara wangu kwa muda utakao wekwa ili nikishindwa kulipa basi dhamana yangu ichukuliwe na pengine kama adhabu pale NSSF nao wakate fungu lao.
Au mifuko yenyewe kwanini isiweke Sheria au utaratibu flani watu waweze kukopa kupitia dhamana za hela zao zilizopo kwao ili jamii ziweze kujikwamua? Tena ikibidi wanaweza kuweka na ka riba flani ila nao wapate faida. Naona umasikini ni mwingi kwa walioajiriwa na wakati mtu ana hela NSSF ya kutosha. Rafiki yangu Mmoja ana milioni 40 NSSF na Leo anahangaika Hana ada ya mtoto wake.
Tunahitaji viongozi flani hivi wanaenda extra mile kutatua matatizo jamii zetu