Tusijadili hii ishu kwa wepesi sana.
Ndani ya ndoa kuna mgawanyo wa majukumu na kila mwanandoa huwajibika.
Ikitokea mke/mume anataka pesa za kutimiza yale majukumu yake au anataka pesa kwa kitu fulani, kuna namna mbalimbali za kupata uwezesho kutoka kwa mwenziwe.Mimi kwa mfano, nikihitaji pesa kiasi fulani na kumwahidi mwenzangu kuwa nitamrejeshea, basi nachukulia huo ni mkopo na huwa narudisha.Hata na yeye hivyp hivyo.Ila pale ninapomuomba anipe kiasi fulani bila kuahidi kurudisha basi hiyo ni grant haihitaji kurejesha.Na yeye ni hivyo hivyo.Tusichanganye mambo jamani.
Kwenye ndoa ipo mikopo, ruzuku na grants.
Ikiwa maneno ya rejareja yanatokea, basi hiyo ni tabia mbaya tu ya huyo msema hobyo.Mwanaume ujilaumu kuoa mwanamke mwenye maneno ya ovyo.