SoC02 Mikopo ya 10% isiyo na riba kwa vikundi vya wajasiliamali. Mapungufu na ufumbuzi

Stories of Change - 2022 Competition

ismaelmkay

New Member
Joined
Aug 25, 2022
Posts
4
Reaction score
2
Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatenga 10% ya mapato yakekwajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya wajasiliamali vijana, wanawake na watu wenye ulemavu nchinzima. Sheria inayosimamia mikopo hii inatoa mwongozo kwa watendaji husika kuhusu kusimamia upatikanaji wa fedha kwaajili ya kutoa mikopo . Watendaji wanasimamia pia usambazaji wa mikopo na urejeshaji wake.

Vikundi vya wajasiliamali vinalengwa na Serikali kwasababu nyakati za kiuchumi haswa njia za upatikanaji fedha kwajili ya kujiendeleza zinawatenga. Huu mkopo upo kama suluhu yakutatua changamoto hii.

Nimefuatilia mkopo huu kwa muda wa miezi miwili na nimeshuhudia utoaji na usimamizi wake. Mapungufu katika mpango huu yanatokana na kanuni ambazo hazija gusa kikamilifu maeneo mengi ya muhimu. Pia mkopo huu unaweza usiwanufaishe walengwa kwasababu wanashindana na wengine wanaotumia mkopo huu kama mbadala. Bila kusahau uhaba wafursa na upungufu wa ujuzi wa ujasiliamali hapa nchini.

Kanuni hizi zinaelekeza kwamba wenye nia ya kupokea mkopo wanatakiwa kuwa wanajishughulisha na ujasiriamali au wanakusudia kuanzisha shughuli za ujasiriamali mdogo au wakati. Lakini wakati wa mchakato wa ukaguzi ili kikundi kipitishwe, kikundi kinatakiwa kiwe na eneo ambapo kinafanyia kazi zake linalokubalika. Hii ni changamoto kwa wale ambao hawana mtaji wa kuanzisha mradi kabisa na wangestahilikupatiwa mkopo.

Changamoto nyingine ipo kwenye suala la urejeshaji wa mkopo ambao umekuwa hauridhishi. Watu wanachukulia poa sana urejeshaji wa huu mkopo. Kanuni zinazoelekeza kuhusu urejeshaji zinaacha nafasi kubwa kwa watu kutokurejesha au kutokurejesha kwa wakati. Waliopokea mkopo wanatakiwa kuanza kurejesha mkopo baada ya miezi 3 toka walipopokea mkopo na kila mwezi baada ya hapo. Hamna kikundi kilichofuata utaratibu huu na sababu zao ni nyingi. Hali ni mbaya, malighafi zimepanda bei na uchumi mbovu. Kuna utaratibu unaofuatwa baada ya kufika hatua hii. Shida kubwa ni kanuni hazimweki mnufaika katika hali ya kuheshimu pesa hizi.

Napendekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa ziwe na mamlaka ya kuanzisha minada ya mali za biashara zinazoendeshwa kwa mkopo huu. Pia nashauli kuwepo mpango wa kufuatilia “balance sheets” za biashara zinazoendeshwa kwa mkopo huu. Balance sheet hizi zinaonesha kiwango cha mkopo kikundi kilichopokea, matumizi ya fedha na mapokezi ya fedha. Kwanza wanufaika wote waliojisajili kwenye kikundi kilichopokea mkopo waelimishwe kuhusu balance sheet na kazi yake. Pili kwa kuambatanisha na taarifa za benki, mweka hazina wa kikundi awasilishe balance sheet ya biashara ya kikundi kwa afisa maendeleo kila mwezi kwa mda ambao mkopo unalipwa. Hii itasaidia kufahamu kwamba biashara kweli ipo inaendelea, na fedha zinatumika hipaswavyo.

Changamoto nyingine ni uhaba wa fursa za kibiashara ambazo tunategemea vikundi vizichukuwe ili kuutumia mkopo huukujinufaisha. Hii inasababisha vikundi vingi kushindwa kurejesha mkopo. Masomo ya uchumi yanaelekeza kwamba ni bora kukopa ili kuendeleza kile ambacho tayari unakifanya naunauhakika wa marejesho yake. Hii unakusaidia kujipima urejeshaji wako na kiasi gani utafaidika. Watu wengi huchukuwa mikopo kwa kutarajia watapata na wengine hushawishika na pesa. Lakini ikifika mda wa kutekeleza miradi na kuanza marejesho ndo wanaona kwamba si kazi ndogo. Vikundi vingi nimeshuhudia vinaomba kubadili miradi vingine huomba kuongezewa mda kwa sababu ambazo wanasema walishindwa kuzitabiri. Hii inaleta mazingira ambayo wale pekee ambao wanaweza kufaidika na kurejesha ni wale walio tulia vizuri tayari kwenye biashara zao.

Chini nimeweka mfano wa mkopo na urejeshaji unaotakiwakikundi kikipokea mkopo huo.
MKOPOMAREJESHO KWA MWEZIMAREJESHO KWA MWAKAFAIDA 30%(MWAKA)FAIDA 40%(MWAKA)FAIDA 50%(MWAKA)
20,000,000833,333(MIAKA 2)9,999,9966,000,0008,000,00010,000,000
555,555(MIAKA 3)6,666,660
50,000,0002,083,333(MIAKA 2)25,000,00015,000,00020,000,00025,000,000
1,388,889(MIAKA 3)16,666,667

Kwa mahesabu yanayoonyeshwa hapo juu, inaonekana ni kwahali gani biashara inatakiwa kuendeshwa ili faida ipatikane. Kufaidika ata kidogo, biashara inapaswa iingize faida kwa 40% au zaidi na mkopo ulipwe kwa mda wa miaka 3 au zaidi. Tunatakiwa tupate suluhu kwa hili jambo la urejeshaji mapema ili badae lisitumike na Serikali kama kisingizio cha kufutampango huu.

Napendekeza Serikali iruhusu makampuni na biashara ziweze kupokea huu mkopo bila riba lakini kwa kutoa ahadi ya kuajiri watu wengine kutoka kwenye haya makundi. Hii fedha ikipatiwa kwa biashara zilizosimama, ikatengwa kwa mfano 12% ikawa kama riba kwa mkopo huu. Hii 12% ikatumika kamasehemu ya kuwapatia watu kwenye hivi vikundi fursa ziwe za kibiashara au kama ajira. Kwa mfano, biashara ikipatiwa mkopo wa milion20, ilazimike kutoa laki2, ambayo iko sambamba na marejesho ya mwezi, kwa mwezi kama mshahara kwa vijana. Hii inaweka fedha hizi moja kwa moja mifukoni mwa hawa watu bila mzigo wa mkopo. Njia njema ya kuwanufaisha hawawatu hasa wale wanaotafuta kutengeneza au kukuza mitaji lakini wanachangamoto ya kuona fursa si kwa kuwapa mkopo iliwaanze kuangaika na fursa za uwekezaji. Ni kwa kuwatengenezea fursa za ajira zilizo rasmi ambazo zitawapatia kipato.

Zaidi ya hapo, nilibaini kuwa asilimia kubwa ya vikundi vilivyoomba mkopo huu vilikuwa ni vya wanawake na vichache vya vijana. Ambapo wengi kwenye vikundi vya vijana ni wanaume. Sikushuhudia kikundi cha walemavu kinaomba mkopo na nivichache vilivyopokea. Tutahitaji msaada kutoka kwa wanasaikolojia kuhusu kwanini wanaume wanasita kuungana haswa kwenye maswala ya kupata pamoja. Kanuni zinaelekeza mgawo wa fedha ambao unatoa aslimia 40 kwa ajiliya vikundi vya wanawake, 40 kwa vikundi vya vijana na 20 kwa vikundi vya watu wenye ulemavu. Naishauri Serikali itoe uhuru kwa maafisa maendeleo ya jamii waweze kubadili mgao waasilimia za fedha hizi ili vikundi vyote vilivyoomba na kukidhi vigezo viweze kupata huu mkopo. Hasa wakati kuna mwitikousio sawa katika vikundi.

Kwa kumalizia, naishukuru Serikali kwa kutoa mpango huu ambao unawasaidia wananchi wengi. Lakini ili huu mpango uendelee vizuri uko mbele napendekeza pia iundwe bodi maalum ya nchi nzima ya kusimamia upatikanaji, utoaji na urejeshaji wa hii mikopo. Hii bodi ifanye kazi na Kamati ya Huduma za Mikopo katika kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ilikuweka msimamo wa kitaalam zaidi.

Kuwepo hifadhi data ya wajasiliamali ambao itakuwa kama mchujo wa yupi anufaike na yupi si mlengwa wa mipango kama hii.

Kuna matukio ya kuingiliwa kwa mchakato wa maombi yamkopo na kupitishwa kwa vikundi. Ambao unaingiliwa na wanasiasa. Hili linafanya utendaji kazi wa maafisa husika kupata changamoto na linapaswa kuangaliwa na kamati za maadili.
 

Attachments

Upvote 4

Sawa naiangalia ndugu.
 
naomba kuuliza kwa mfano hamjarejesha hizo hela mlizokopa mnaweza kuwapa rasilimali zenu wafidie deni??
 
Kwasasa uwo sio utaratibu unaofuatwa. Sasa hivi ni pesa tu
Lakini si nasikia huwa kuna dhamana ya mali unayoiweka kama ushahidi wa mali unayoimiliki?

Sasa ukishindwa kulipa si wana deal na hiyo mali au mi ndio sijaelewa?
 

Naomba kujuzwa je kiwango cha mkopo katika mikopo hii huwa minimum ni Tsh ngapi kwa kikundi, na maximum ni Tshs. ngapi?

Naona kanuni ziko kimya hazijasema hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…