Tetesi: Mikopo ya 10% ya Halmashauri imegeuka kuwa mikopo ya Wanachama wa CCM

Tetesi: Mikopo ya 10% ya Halmashauri imegeuka kuwa mikopo ya Wanachama wa CCM

Habari wana jamvi.

Naomba kuwasilisha mada hii kuviomba vyama vya Upinzani vipaze sauti kuhusu utaratibu mbovu ambao kwa sasa Halmashauri nyingi Nchini wanafanya kutoa mikopo kwa kigezo cha kuwa mwanachama wa CCM hasa vikundi vya wanachama wao ndivyo vinapewa mkopo.

Niko Mkoa x na ninafanya kazi katika vitengo ambayo vinapelekea kupata taarifa hizi. Mwaka juzi waliondoa majina ya baadhi ya wanakikundi ambao kwa maelezo yao walikuwa na mlengo wa kisiasa tofauti baada ya kupewa maelekezo na diwani wa eneo husika kuwa ikiwa watawaweka watu hao wasahau kuhusu mkopo na kama wanahitaji mkopo wawatoe haraka kwenye kikundi.

Kwa uelewa wangu ni kuwa fedha za 10% ya mikopo ya Wanawake, Vijana na Wazee ya Halmashauri ni fedha ambayo inatolewa na Serikali ikiwa ni mapato yatokanayo na kodi za wananchi wote pasipo kujali vyama wala itikadi zao na fedha hizi HAZITOLEWI NA CHAMA CHA CCM kwenda kwa wanachama wake.

Hivyo Serikali kupitia watendaji wake wanasimamia na kuratibu mambo haya ambayo yakiachwa baadae yatakuja kuleta athari kubwa hata mgawanyiko katika jamii.

Nawasilisha
kwani ulikua hujui? we uliona wapi mkopo mpaka wahakiki kadi yako ya uanachama , habari ndio hiyo haiwezekani wezi wagawie hela watu wasio wezi wenzao never
 
kwani ulikua hujui? we uliona wapi mkopo mpaka wahakiki kadi yako ya uanachama , habari ndio hiyo haiwezekani wezi wagawie hela watu wasio wezi wenzao never
Tuna safari ndefu ya mabadiliko
 
Back
Top Bottom