Program Manager
JF-Expert Member
- Aug 6, 2018
- 2,763
- 3,955
Mimi ni kijana Mjasiriamali,miongoni mwa vijana wanaostahili kupata mikopo hii kwani Ninakidhi vigezo vyote.
Lengo la kutoa mikopo hii lilikuwa ni kutuwezesha sisi wajasiriamali kuinuka kiuchumi na kuinua mitaji yetu.
Changamoto ni kwamba tunaunda vikundi ,tunaandaa katiba na vielelezo vyote vinavyohitajika Kwa kutumia pesa zetu zile zile za mitaji midogo tunayodunduliza halafu Mchakato wa kuhakikiwa na kupewa mikopo unachukua muda mrefu sana mpaka wengine wanafilisika kabisa.
Ngazi ya Halmashauri kumekuwa na dalili za upendeleo na kujuana Ili kikundi kiweze kunufaika na mkopo,hii siyo afya kwani husababisha watu wenye sifa kukosa fursa hii.
Ushauri.
Mikopo itolewe bila upendeleo Wala kujuana.
Mikopo itolewe Kwa wakati kabla mtu hajasahau wazo lake la biashara.
Mikopo itolewe Kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja ikiwa anakidhi vigezo tofauti na Sasa ambapo inatolewa Kwa vikundi tu. Faida ni kurahisisha kuhakikiwa Kwa wakati na pia kunufaisha vijana na wanawake wengi wasio na vikundi.
Kusiwe na interval na term ya kutoa mikopo Bali itolewe wakati wote pale tu mtu anapokamilisha na kukidhi vigezo.
Naomba niishie hapa kwanza nawahi kuifungua kibanda changu Cha nyanya.