Mikopo ya Bajaji na Pikipiki ni komesha!

Mikopo ya Bajaji na Pikipiki ni komesha!

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
Leo nimepita Sabasaba nikaona kuna Kampuni fulani (Jina Kapuni) inatoa mikopo ya Pikipiki na Tukutuku.

Mjanja M1 nikajisogeza taratibu kuokota Dodo la mkopo wa Bajaji.

Lahaullah Walakuwata! nilishtuka sana kuambiwa marejesho ni zaidi ya ulichokopa, yani kama umekopa 10 Million wanakutaka urejeshe 21 Million.

Nikawaambia Asanteni sana na nikatoka Nduki mithili ya Hussein Bolt wa Jamaica.

WATOA MIKOPO WANAWAKOSEA SANA WATANZANIA.
 
Mkopo wowote unakuwa na interest. Interest inategemea muda wa kurejesha na rejesho kwa kila mwezi. Kadri muda unavyokuwa mrefu na unavyo rudisha kidogo kwa mwezi ndo riba itakavyo kuwa kubwa.

So usitegemee ukope Tsh 1m to Urejeshe shs 1m. Au usitegemee aliyerudisha ndani ya mwaka mmoja alipe riba sawa na anayerudisha kwa miaka 3.

Cha msingi ni kuelewa vigezo na masharti n kuangalia kama unayamudu unakopa na kama huyamudu unaacha nao.
 
Leo nimepita Sabasaba nikaona kuna Kampuni fulani (Jina Kapuni) inatoa mikopo ya Pikipiki na Tukutuku.

Mjanja M1 nikajisogeza taratibu kuokota Dodo la mkopo wa Bajaji.

Lahaullah Walakuwata! nilishtuka sana kuambiwa marejesho ni zaidi ya ulichokopa, yani kama umekopa 1 Million wanakutaka urejeshe 2.1 Million.

Nikawaambia Asanteni sana na nikatoka Nduki mithili ya Hussein Bolt wa Jamaica.

WATOA MIKOPO WANAWAKOSEA SANA WATANZANIA.
Ni wale wanaojiita people au Wale Wanaojiita Diamond
Nilikua na mpango mwezi wa nane nikakope Bajaj
Duh
 
Mm niliulizia Bajaji wakaniambia unarejesha 21 Million kwa Two Years mpaka nikataka kucheka.

Sijajua kuhusu Bodaboda, ila naamini wanacheza humohumo kwenye ukandamizaji.
Kudadeq. Bahaji mpya Mil 10-11 so karibia 100% interest.

Kwa wanaosema jaribu Bank ukione xha moto, Ukichukua Mil 11 CRDB kwa miaka miwili unalipa Mil 12 na nusu.

Screenshot_20240708-193146.png
 
Back
Top Bottom