Mikopo ya BAYPORT

Mikopo ya BAYPORT

Wazo . ..miaka 3 ukiweka kidogo kidogo utakuwa na 5.5 bila riba.

Sasa haraka ya nini. ..5.5 unapata nyumba lindi?

Ogopa matapel. ..ukumbuke kuja kuleta mrejesho
 
benki zinazingua sana siku hizi mpaka watu wanaangukia kwa matapeli, zile benki za vijijini nmb, crdb, posta ukifanya mchezo unakaa miezi 2 unangoja mkopo, byport wiki haiishi ndio maana wanawapataga

Humalizi wiki umeshapata pesa labda utachelewa kufanya process kwa mwajiri wako maana ana sehemu yake ya kusaini
 
Bado hatujapewa barua ya uthibitisho kazin mpaka one year!

barua yko ya kuajiliwa sio ya kuthibitishwa...wao NMB wanaweza wakaupa ili mradi uwe na salary slips za miezi mitatu mfululizo ya kalibuni na iyo barua yko ya ajira wanaweza kukupa ata bila ya kuthibitishwa labda wakompliketi
 
Usiende kwa hao jamaaa Utalia ww acha kabisa kuwafikiria acha! acha! ww
 
Natumai hamjambo waungwana,mimi ni mwajiriwa serikalini,sijathibitishwa kazini bado,hoja yangu ni kutaka kuchukua mkopo kupitia bayport kiasi cha sh miliion tano na nusu,na nataka kuurejesha ndani ya miaka mitatu,take home yangu ni sh laki tano.je itanigharimu kiasi gani mpaka kuukamilisha kwa muda huo wa miaka mitatu? Naomba msaada na changamoto za hawa jamaa wa bayport,lengo la mkopo ni kununua nyumba.

Nenda CRDB salary slip za miezi mitatu tuuuu unapewa mkopo achana na matapeli hao....
 
Tulia kwanza kijana. Na nakushauri USIKIMBILIE KUKUPO kwenye hizo taasisi UTALIA ndugu yangu. Mikopo ya faidika,blue fanancial bayport weka mbali na watoto....USITHUBUTU.
 
C.W.T INAENDESHA KESI DHIDI YA BAYPORT KWA KUWABAMBIKIA RIBA KUBWA TOFAUTI NA MAKUBALIANO, SASA BADO KINA WATU WANAWAZA TENA BAYPORT!!!
YATAKAYO KUKUTA RUDI HAPA UTUJULISHE okonwo jr@
Asante mkuu,nilienda bay port riba kwa 5 mls=13mls kwa miaka mitano,sikuchukua,nimeona ni wizi hakika
 
hivi kwa mfano ukakopa hiyo m 5 halafu ukafanikiwa kuwekeza kitu ambacho baada ya hiyo miaka mitatu kitakupa faida ya zaidi ya Hayo m 15 watakayokata,hasara iko wapi?
Ishu ni kuchukua mkopo kwa malengo na siyo kukurupuka
Kama wote tungekuwa na akili za kujumlisha kama hizi nazani huenda rais Wa nchi angepita White hairs
 
Nenda NMB,POSTAL BANK& CRDB wanakupa mkopo siku hizi Hawahitaji Confirmation letter.Mimi niliwasiliana nao llast month na ndani ya wiki unaweza chukua chako hususan NMB wameimprove sana nowdays.
 
Hao n wakuogopwa kama UKOMA, nenda bank unapata mkopo kiulaini tu
 
Wengi wanao ona mikopo mibaya ni wale walio enda kopa bila kuwa na sababu maaalumu
Au wamekopa hela ila si kwa shughuli itayozalisha hizo hela

Mtu anakopa ili akajenge
Mtu anakopa ili anunue gari
Mtu anakopa ili afunge ndoa
Mtu anakopa ili tu nae awe kati ya waliokopa

Tukikopa kwa staili hizi huwezi fika mbali kamwe
Mikopo ni kwa wafanya biashara pekee maana zinajizalisha
 
bayport iogope kama UKIMWI tunavyouogopa kama huogopi ukimwi nenda kakope baada ya kukopa ulete mrejesho hapa wa cd4 zimebaki ngapi
 
Asanteni, mmenifungua! Bayport wameshanipigia simu sana kunibembeleza nikope kwao.
 
Achaneni na kukopa bank au huko Bayport. Nendeni mkakope Saccos.
 
Back
Top Bottom