SoC01 Mikopo ya Biashara ya Vijana Serikalini

Stories of Change - 2021 Competition

flulanga

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2016
Posts
4,860
Reaction score
6,390
Serikali kupitia mapato ya halmashauri kumekuwepo na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya mikopo kwa vijana na watu wenye ulemavu.

Wimbi kubwa la vijana kulalamika ukosefu wa ajira na ukosefu wa mitaji ya biashara, kilimo na shuuri nyingine za kuwaingizia vipato hii ndio ilikuwa suluhisho endapo kama ingetumika vyema.

Kumekuwepo na habari kuhusu utoaji wa hiyo mikopo lakini uchangamfu wa vijana kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo imekuwa ndogo. Na serikali imekuwa haitoi elimu hiyo.

Naongelea uhalisia wangu mimi kama kijana. Ishawahi kumvaa mkuu wa mkoa na akanielekeza niende kwa muhusika na namba yake nikapewa. Nilimpata muhusika na muongozo mzima alinipatia, nikarudi mtaani ili niweze kufanya kile nilichoelekezwaaa.

Niliambiwa nifanye haya;

- Niunde kikundi cha watu kuanzia wa tano,

- Tuchague uongozi wa muda,

- Tuunde katiba yetu ambayo ndio utakuwa muongozo wetu,

- Tuchague uongozi kulingana na katiba tuliyoiunda,

- Tuanzishe mradi wowote kama ni kilimo au ufugaji, au biashara, au hata kiwanda kidogo.

- Na mwisho tufungue akaunti bank.

Baada ya vyote hivyo twende kwa afisa mtendaji wa eneo letu kupitia kwa mwenyekiti wa mtaa kwaajili ya kupatiwa barua ya utambulisho twende nayo halimashauri kwaajili ya hatua nyingine zaidi.

Niliporudi mtaani ili niunde hicho kikundi cha watu kuanzia watano ndipo nilipogundua vijana wengi hawana muamko kuhusu hii mikopo ya serikali. Wengi ambao nilihisi nikiwapelekea hili wazo watalichangamkia ila kwa bahati mbaya ikawa kinyume chake. Kila mtu alitoa neno lake analolijua yeye;

Kuna mwingine alisema 'serikali haiwezi kutoa pesa zake zaidi watatupotezea muda wetu bure'

Mwingine akasema ' hiyo mikopo inatoka kimjuano'

Mwingine akasema 'hatuwezi kupata pesa mpaka nasisi tuwe na pesa ya kuweka kwenye akaunt kwahiyo yeye hana hiyo pesa.

Na wengine walitoa kauli zakufanana na hizo. Na mwisho wa siku nikapata kijana mwenzangu mmoja tu kwahiyo kigezo cha kwanza cha kuwa na kikundi cha vijana watano kikatuangusha.

Nini kifanyike ili vijana waielewe hii fursa;

- Halimashauri zitenge muda wa kukutana na vijana na kuwapatia elimu kuhusu hii mikopo na iwahakikishie kuwa mikopo ipo na wala sio uraghai kama vile baadhi ya vijana wanavyoamini.

- Serikali za mitaa iwe na orodha ya vijana wanaojitambua na ambao tayari wameshaanzia chini na hatua waliofikia wanahitaji kuwezeshwa kupitia hiyo mikopo. Hii itajenga uhakika wa marejesho ya mkopo husika.

- Serikali ianze kutoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja kama vile ilivyo mikopo ya chuo elimu ya juu. Hii itapelekea kijana kupambana na marejesho yake bila kuhisi kuwa akikwama yeye basi wenzie watamlipia kupitia kikundi chake. Hili lilinikwamisha baada ya kukosa vijana wenzangu ila pangekuwepo na mkopo wa mtu mmoja mmoja uenda labda ningepata mkopo.

- Serikali itoa mikopo kwa wakati. Pamekuwepo na malalamiko mikopo ya serikali haitoki kwa wakati kama mlikuwa na wazo la biashara basi mpaka wazo hilo litapitwa na wakati ila mkopo bado.

- Mikopo itolewe kwa biashara ya mtu mmoja mmoja na wala sio kwa kikundi ili kukwepa vijana kutokuaminiana. Hii miradi ya vikundi pamekuwepo na kuzurumiana sanaaaa kwa baadhi ya wanakikundi kutokuwa waaminifu kwahiyo serikali iliangalie hili.

MWISHO; Serikali itoe elimu ya mikopo ya biashara kwa vijana kama vile inavyotoa elimu kuhusu uombaji wa mikopo ya elimu ya juu. Na vijana tuchangamkie fursa hizi na kama kuna vikwazo katika upatikanaji wa hii mikopo basi ni bora tukajionee wenyewe kuliko kusikiliza habari za mitaani.
 
Upvote 13
Mimi kwa uzoefu wangu hiyo mikopo imejaa siasa kuliko uhalisia. Nilipomaliza chuo nikarudi mtaani kwa speed sana na waskaji kumfuatilia huo mchongo.tukaanza na kupata taarifa kutoka ngazi zote zinazohusika, kutoka hapo tukaanzisha kikundi,tukakisajiri Safi, tukakaibua mradi mzuri sana unaohusisha kilimo(horticulture),tukatafuta eneo Sasa shida ikaja kwenye kupata huo mkopo ilikua ni nenda rudi nyingi Sana tukaja kugundua ile mikopo wanapeana wenyewe mfano madiwani wanatengeneza kikundi hewa wanachukua mkopo wanatulia sisi vijana na kinamama walionje ya ule mfumo hampati yaani naondoka hakuna kitu mpaka leo nikiangalia documents zile nacheka hasa ninapoona wanahamasisha vijana na kinamama nabaki nacheka tu
 
Ni kweli baadhi ya maeneo hili ni tatizo. Kwanini msingemtumia diwani wa eneo lenu labda ingekuwa rahisi
 
Tena huyo ndio muongo kweli alikua anatutumia kwenye siasa zake, tulimuona mkuu wa wilaya, DED na mwenyekiti wa halmashauri tuliishia kusifiwa tu kuwa andiko letu zuri tu
 
Serikali kupitia mapato ya halimashauri kumekuwepo na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya mikopo kwa vijana na watu wenye ulemavu.

Wimbi kubwa la vijana kulalamika ukosefu wa ajira na ukosefu wa mitaji ya biashara, kilimo na shuuri nyingine za kuwaingizia vipato hii ndio ilikuwa suruhisho endapo kama ingetumika vyema.

Kumekuwepo na habari kuhusu utoaji wa hiyo mikopo lakini uchangamfu wa vijana kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo imekuwa ndogo. Na serikali imekuwa haitoe elimu hiyo.

Naongelea uhalisia wangu mimi kama kijana. Ishawahi kumvaa mkuu wa mkoa na akanielekeza niende kwa muhusika nanamba yake nikapewa. Nilimpata muhusika na muongozo mzima alinipatia, nikarudi mtaani ili niweze kufanya kile nilichoelekezwaaa.

Niliambiwa nifanye haya;

- Niunde kikundi cha watu kuanzia wa tano,

- Tuchague uongozi wa muda,

- Tuunde katiba yetu ambayo ndio utakuwa muongozo wetu,

- Tuchague uongozi kulingana na katiba tuliyoiunda,

- Tuanzishe mradi wowote kama ni kilimo au ufugaji, au biashara, au hata kiwanda kidogo.

- Na mwisho tufungue akaunti bank.

Baada ya vyote hivyo twende kwa afisa mtendaji wa eneo letu kupitia kwa mwenyekiti wa mtaa kwaajili ya kupatiwa barua ya utambulisho twende nayo halimashauri kwaajili ya hatua nyingine zaidi.

Niliporudi mtaani ili niunde hicho kikundi cha watu kuanzia watano ndipo nilipogundua vijana wengi hawana muamko kuhusu hii mikopo ya serikali. Wengi ambao nilihisi nikiwapelekea hili wazo watalichangamkia ila kwa bahati mbaya ikawa kinyume chake. Kila mtu alitoa neno lake analolijua yeye;

Kuna mwingine alisema 'serikali haiwezi kutoa pesa zake zaidi watatupotezea muda wetu bure'

Mwingine akasema ' hiyo mikopo inatoka kimjuano'

Mwingine akasema 'hatuwezi kupata pesa mpaka nasisi tuwe na pesa ya kuweka kwenye akaunt kwahiyo yeye hana hiyo pesa.

Na wengine walitoa kauli zakufanana na hizo. Na mwisho wa siku nikapata kijana mwenzangu mmoja tu kwahiyo kigezo cha kwanza cha kuwa na kikundi cha vijana watano kikatuangusha.

Nini kifanyike ili vijana waielewe hii fursa;

- Halimashauri zitenge muda wa kukutana na vijana na kuwapatia elimu kuhusu hii mikopo na iwahakikishie kuwa mikopo ipo na wala sio uraghai kama vile baadhi ya vijana wanavyoamini.

- Serikali za mitaa iwe na orodha ya vijana wanaojitambua na ambao tayari wameshaanzia chini na hatua waliofikia wanahitaji kuwezeshwa kupitia hiyo mikopo. Hii itajenga uhakika wa marejesho ya mkopo husika.

- Serikali ianze kutoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja kama vile ilivyo mikopo ya chuo elimu ya juu. Hii itapelekea kijana kupambana na marejesho yake bila kuhisi kuwa akikwama yeye basi wenzie watamlipia kupitia kikundi chake. Hili lilinikwamisha baada ya kukosa vijana wenzangu ila pangekuwepo na mkopo wa mtu mmoja mmoja uenda labda ningepata mkopo.

- Serikali itoa mikopo kwa wakati. Pamekuwepo na malalamiko mikopo ya serikali haitoki kwa wakati kama mlikuwa na wazo la biashara basi mpaka wazo hilo litapitwa na wakati ila mkopo bado.

- Mikopo itolewe kwa biashara ya mtu mmoja mmoja na wala sio kwa kikundi ili kukwepa vijana kutokuaminiana. Hii miradi ya vikundi pamekuwepo na kuzurumiana sanaaaa kwa baadhi ya wanakikundi kutokuwa waaminifu kwahiyo serikali iliangalie hili.

MWISHO; Serikali itoe elimu ya mikopo ya biashara kwa vijana kama vile inavyotoa elimu kuhusu uombaji wa mikopo ya elimu ya juu. Na vijana tuchangamkie fursa hizi na kama kuna vikwazo katika upatikanaji wa hii mikopo basi ni bora tukajionee wenyewe kuliko kusikiliza habari za mitaani.
Hizi pesa zpo kweli kwa mfano uku halmashaur ya kwetu wanaimiza vijana tuunde vikundi. ila chang'amoto ni apo kwenye vikundi. watanzania atupendi ka-share biashara yani tupenda kutoboa pekee pekee. na hata vikundi ambavyo vimeundwa wakishapata hela wanagawan kila mtu anaenda kufanya anacho jua mwenyewe.
 
Ni kweli kwenye upande wa vikundi ni changamoto ndiomaaana hapo juu nimeshauri wangeanzisha na mikopo ya mtu mmoja mmoja.
 
Tena huyo ndio muongo kweli alikua anatutumia kwenye siasa zake, tulimuona mkuu wa wilaya, DED na mwenyekiti wa halmashauri tuliishia kusifiwa tu kuwa andiko letu zuri tu
Hilo ni tatizo, wakiondoa ukiritimba kama huo naamini mikopo hiyo ingesaidia wengi sanaaaa vijana
 
Maoni mazuri sana,hakuna jambo kama hilo likakosa changamoto. Ukweli kama wewe siyo kada utasubiri na huo ndo ukweriii
Nadhani haya mambo yakiendeshwa kwa uwazi basi habari hizo za ukada tusingezisikia.
 
Mimi na wenzangu kumi ni wanufaika wa mkopo huo Tsh 20 ml haikua kazi rahisi tumefungua mradi wa ufyatuaji tofali
Hapo juu naona kuna baadhi ya wachangiaji wanaongelea ukada wa chama tawala.

Vipi nyie kwa upande wenu? Je iliwabidi muwe makada kwanza ndio mpate/mkapata mkopo?
 
Hii mikopo ipo hila tatizo ngozi nyeusi si waaminifu.
Nakumbuka mwaka fulani tuliungana vijana watano, hasa lengo ni huu mkopo.
Tulihangaika sana kuupata maana vikundi vilikua ni vingi. Mungu si athuman tukatoboa m10. Tukafanya mgao kila mtu apate m1 ya shughuli zake(jumla 5m), hii 5m tuanzishe mradi wa kutupa hela za marejesho na kuiweka iwe ajira kwetu.
After hapo [emoji28][emoji28][emoji28] tukaanza bata[emoji28][emoji28] kilichokuja kutokea [emoji17] kundi likavunjika, ulipaji wa deni ukawa mzigooo na baadhi walikimbia wachache (2) tukabeba dhamana ya kulipa ...

Hii kikundi ni heri muwe familia.
 
Ushuhuda mzuriiii... Upande wa vikundi ndio tunaangushana hapo.

Vipi kuhusu ukada wa chama. Hapo juu kuna wachangiaji wanasema ukada kwanzaaa!!! Vipi kwa upande wenu
 
Hapo juu naona kuna baadhi ya wachangiaji wanaongelea ukada wa chama tawala.

Vipi nyie kwa upande wenu? Je iliwabidi muwe makada kwanza ndio mpate/mkapata mkopo?
Hapana sisi ni raia wa kawaida tu ambao tuliiona hiyo fursa na kuifanyia kazi.

Na Afisa maendeleo kata na wilaya walitupa support bila kudai chochote

IMG-20210626-WA0025.jpg
 
Hapana sisi ni raia wa kawaida tu ambao tuliiona hiyo fursa na kuifanyia kazi.

Na Afisa maendeleo kata na wilaya walitupa support bila kudai chochote

View attachment 1879029
Aha sawaaa, ushuhuda mzurii sanaaaa. Vijana tupambane tuache mawazo ya ukada. Inawezekana kupata mkopo bila ukada ushuhuda huu
 
Ushuhuda mzuriiii... Upande wa vikundi ndio tunaangushana hapo.

Vipi kuhusu ukada wa chama. Hapo juu kuna wachangiaji wanasema ukada kwanzaaa!!! Vipi kwa upande wenu
Hili la ukada nakiri lipo, na linakuwepo kwasababu ya kuharakishiwa jambo lenu.
NB: Ni sehemu hadi sehemu
 
Back
Top Bottom