Mikopo ya bure kutoka ''Tala' Hongera lakini kuwa makini na wabongo!

Acheni kutuharibia... Wengine tunakopa vizuri tu na kurejesha japo ni pesa ndogo ndogo.. Mkiletewa urahisi mnadai Igumu, mkiletewa ugumu mnalalamika... Duh wabongo hawaeleweki... Badala ya kukopa huko na urejeshe unatafuta kuwambia hatari iliyopo ...washafanya Risk analysis ...so waache wafanye kazi... Kuna sehemu nishsona wadaiwa sugu wanaorodheswa kwenye kampuni za ufilisi, wao ndo watakutrace tu.. Pia si kila ukiwa na FB account watakupa mkopo, wengine wanakataliwa. Ila tujifunze uaminifu inapotokea fursa hizi.
 
Siku ya kwanza kuona hii kitu...niijisemea moyoni kuwa hawa jamaa hakika watalia sana
Hakika watajuta kuja Kwa Watanzania sisi
Kuna watu kama 10 nao wafahamu wamepata hawalipi na hawana mpango wa kulipa
 
usiwakumbushe nimekula laki mbili yao sahivi sipatikani line nimeifungia kabisa na sina mpango wa kuwalipa
 
Kimsingi inasaidia sana. Kuna siku kiukweli, hangaika hangaika zangu kikawaida ziligonga mwamba, nilikuwa nahitaji 50,000. Kwa jamaa na ndugu nilikosa, nikakumbuka nilishawahi kopa TALA, nilifikishaga 40,000; nikawacheki tena, aisee, nilipewa mkopo wa 60,000. niliokolewa na huo mkopo. So ni vizuri kuwazoea taratibu, ila usikope nyinginyingi maana riba ya 20% si haba. yaani fanya iwe ni kimbilio kwenye uhitaji wako wa faster, najua wengine watasema kiasi kidogo kinachotolewa hakina faida kiuwekezaji, ACHA hiyo mindset, waza tu siku ulivyowahi kuhaha kutafuta 20,000 na kuaibika hata kumkopa "house girl wako", kumbe ungeingia TALA. Usikope TALA ilihali unayokopa una uwezo nayo, eti ilimradi umekopa uongeze "round pale rombo green view".
 
Nilipokea malipo ya elfu 20 thats why nikaandika humu
Wana riba kiasi gani maana mie hii mikopo kama ya Timiza ya Airtel na Mpawa ya vodacom naipenda japokuwa Timiza kama imekuwa ngumu kidogo kimakato..embu nipe kwa ufupi hiyo riba niongeze taasisi ya tatu ya kukopa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…