Mikopo ya hazina, Maafisa Utumishi wanaomba 10% ili waweze kupitisha

Mwezi mmoja boss.....nimekunja mpunga wangu....mpunga Haina riba....unarudisha uliopewa....kifupi mshahara wako unapewa advance ya nusu ya mshahara wako....yaani unalipwa miaka SITA ijao nusu ya mshahara wako
Bora hii aisee kuliko kwa haya mabenki yenye riba kandamizi.
 
Ni kweli haisikiki kwa Sana....maana SERIKALI ikifanya hivyo mabenk yatafunga OFISI zao. Pia kumbukeni hata mkituma kwenye hazina portal bado harmashauli wanawajadili wakupe au wasikupe kutokana na vigezo vyako....pia mwisho wa siku Ili upate mkopo, ni lazima mkurugenzi apitishe......kwa hiyo maafisa utumishi hawaepukiki ndugu zangu.......ni kuomba mungu....ukipata ni mkopo mzuri
 
Uko wapi huko nihamie, maana Kuna Halmashauri zina watu Wana njaa kaliiiiiiiiiiiio mixer roho za kichawi
 
tatizo nini au ndo maafisa utumishi wanachukua tozo?
 
Mimi nimeomba tangu mwezi Oktoba, lakini hadi sasa hakuna(sijapata). Wazoefu hii mikopo inachukua muda gani hadi upewe?
 
Kauli ya Rais, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni zaidi ya Sheria.
Na Rais ameishatamka kwamba, "KILA MTU ALE KWA UREFU WA KAMBA YAKE"
 
Hapa kwenye postcode, house number, street, address unajaza zipi wadau za kituo ninachofanyia KAZI au sehemu ninayoishi? Naomba msaada
 
Mimi nimeomba tangu mwezi Oktoba, lakini hadi sasa hakuna(sijapata). Wazoefu hii mikopo inachukua muda gani hadi upewe?
Mkuu hapa kwenye address, zip code, house number, street unajaza zako au za mwajiri au za kituo unachifanyia KAZI.
 
Imefichwa sn hii mikopo,si sawa.ipo kwaaajili ya wachache
 
Hapa kwenye postcode, house number, street, address unajaza zipi wadau za kituo ninachofanyia KAZI au sehemu ninayoishi? Naomba msaada
Post code, muulize HR au mkuu wako wa idara,.....house namba ninamba unayoishi, address ni chukua ya kazini kwako,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…