Mikopo ya "Kausha damu" yawakaba koo walimu Mbozi

Mikopo ya "Kausha damu" yawakaba koo walimu Mbozi

sunguramjinga

Senior Member
Joined
May 11, 2023
Posts
175
Reaction score
227
Baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani Mbozi mkoani Songwe, wameomba uwepo wa majukwaa ya mara kwa mara yatakayolenga kutoa elimu ya utambuzi wa Taasisi sahihi za kifedha zinazotoa huduma za mikopo, ili waweze kujiepusha na Taasisi ambazo zimekuwa zikiwakopesha mikopo yenye riba kubwa na kuwasababishia madeni yasiyolipika.

Walimu hao wameyasema hayo katika mkutano maalumu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Mbozi, uliolenga kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo mikopo.

Chanzo: ITV
 
1684127633373.png
 
Tatizo la walimu,
Kukopa wamefanya mazoea,
Ata awe na cash mfukoni,atakopa TU.

Pia hata hasichokihitaji kwa wkt huo, Kwasababu tu kinakopeshwa, atabeba tu.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Duh umenifurahisha mkuu,eti hata asichokihitaji kwa wakati huo,ili mradi kinakoposhwa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Duh umenifurahisha mkuu,eti hata asichokihitaji kwa wakati huo,ili mradi kinakoposhwa [emoji23][emoji23][emoji23]
Kweli kabisa mkuu,

Huku kwenye viband vyetu tunawaona,

Ukiwaambia kinakopeshwa wanabeba.

Hata kiuzwe Mara 4 ya Bei halisi,hawajali wanachukua, changamoto yake Sasa kwny kulipa, UTAJUTA.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ni kampuni za mikopo.
Dhamana ni kadi yako unayochukulia mshahara.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Nimevutiwa na hili. Hawahitaji statement ya uthibitisho kua ndio kadi halisi unayoingiziwa mshahara? Mikopo yao ina range ngapi mpaka ngapi? Vipi riba?

Mkuu husichoke maswali yangu naomba udadavue kidogo unipe mwanga.
 
Back
Top Bottom