Mikopo ya kilimo mkoa wa pwani

Joined
May 24, 2012
Posts
79
Reaction score
56
Wadau,
Kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza umaskini wa kipato kwa wakazi wa mkoa wa pwani endapo watawezeshwa kupatiwa mpenyo wa kupata huduma za kifedha kwa ajili ya kununua pembejeo za kilimo na utaalamu wa uzalishaji mazao hasa ya muda mfupi. Katika utafiti wangu kama mtaalamu wa mambo ya fedha nimebaini kuwa mikopo midogo midogo inaweza kuwasaidia hasa vijana wanaochakarika na kilimo cha matunda na mbogamboga

Nina hitaji msaada kwa mtaalamu wa uandishi wa miradi midogo midogo ya kilimo ili tuweze kushirikiana katika hili. Hata kama sio kushirikiana nina hitaji mtaalamu mwelekezi ambaye anaweza kuniandikia andiko la mradi. Tafadhali nitumie ujumbe au nitumie kwa email chakarikamkopo@yahoo.com

Asante.
 

Unahitaji andiko la mradi wa kulima, kufuga, n.k ??
Andiko liwe la mradi wa ukubwa gani (yaani thamani ya mradi wako ni sh ngapi ???) Tsh. 1 million. Tsh. 5 million, Tsh. 20 million ??
Una shamba / eneo la ukubwa gani ambapo unapanga kuanza shughuli zako za kilimo ??

Tupo pamoja mkuu katika kilimo mkoani Pwani.
 
Nashukuru sana, shida yangu ni mtu ambaye anaweza kunisaidia kuandika proposal ili kuweza kupata fedha za kusaidia wakulima 1,000 kwa kuanzia. Kuna taasisi moja ya kanisa ya Uswisi wamekubali kutoa mtaji wa mzunguko (Revolving Fund) kusaidia vijana wakulima kuendeleza hicho kilimo. Nina hitaji proposal kwa ajili ya kusubmit kwa hao funders
.
 

Okay, ngoja kuna mtaalam wa hizo proposal yuko humu JF.
Anaweza kuja on-line jioni hii.
 

Tupo pamoja sana mkuu chakarikamkopo.
Nimekutumia private message ya maelezo zaidi. Tuwasiliane.
 

mkuu Chakarikamkopo, tunaomba updates za hatua uliyofikia kuhusu kuandika business plans za kilimo.
Naona Roky amewasiliana na wewe kuhusu azma hiyo.
Sisi wote tunasubiria updates toka kwako tujiunge nawe kwenye ujasiriamali huko mkoa wa Pwani.
 
Wasiliana na mdau humu anaitwa Babalao.. ni mweledi katika anga unayoulizia..
 

Vipi mkuu mbona uko kimya sana ??
Tunasubiri response zako.
 
Vipi mkuu mbona uko kimya sana ??
Tunasubiri response zako.

Sitaki kumsema vibaya huyu mwenye uzi, lakini inaonekana anasahau sana. Kuna wakati nilimpelekea mail yangu baada ya yy kuanza,lakini mpaka leo hajarejesha mrejesho, nikadhani kahama nchi, ghafla kaja na uzi huu. Vuta subira mkuu mkuu atakujibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…