Mikopo ya kimkakati ya Ku stimulate uchumi

Mikopo ya kimkakati ya Ku stimulate uchumi

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Kwa mtazamo wangu Mama anafanya Vizuri sana na pia najua kuwa sio kila kitu kinaweza kufanyika kwa wakati mmoja hata hivyo nimeona nichangie yafuatayo;
Ili kuwa na makusanyo ya Kodi makubwa na ya uhakika na kutengeneza ajira nyingi kwa Vijana nafikiri ipo haja ya kutazama upatikanaji wa Mikopo mikubwa ya riba nafuu kabisa (hii mikopo ya ndani ya riba 17 - 20% siamini kama inaweza kutuvusha)
Namaanisha kuanzisa Miradi itakayo ajiri watu wengi, yenye faida na inayo ingizia Serikali Kodi kubwa kwa mfumo wa trickle down effect

Tunaweza kuanza kwa kuforcus kwa bidhaa tunazo nunua Nje kwa wingi; Mfano:
  • Viwanda vya madawa ya watu na Kilimo (tunao wakemia wazuri waliosoma vizuri naamini tunaweza) Nafikiri ndani ya miaka 3-5 hivi hela ya Uekezaji itakuwa imerudi
  • Kiwanda cha kisasa cha kuzalisha matairi ya aina zote kama ilivyokuwa General tire ILA more innovation inatakiwa hapa kwani technology inabadilika. Soko kubwa tunalo nikuamua tu...hata sijui tunakwama wapi
  • Kiwanda kuzalisha Lami/Kusafisha mafuta (tunahitaji Lami, mafuta nk) kwa bei rafiki
  • Kuchakata gasi tuliyo nayo ifae kupikia au pengine kusambaza gesi tuliyonayo kwa watu
  • Kiwanda Kikubwa na cha kisasa cha kutengeneza genuine spae kama ilivyo kuwa Machine tools ILA hapa tunahitaji kiwanda cha kisasa zaidi kiendane na wakati
  • Meli ya kisasa za Uvuvi kwani tuna ukanda mkubwa wa bahari ila hatufaidiki nao
  • Kilimo cha Mazao ya kimkakati na Ranchi za shamba darasa (namaanisha shamba la kuanzia hekari 100 hivi nakuendelea. Tunao Vijana wengi wazuri wa kila idara ya kilimo kutoka pale SUA nk.
  • Kiwanda kikubwa cha Vifungashio vya bei rafiki na wataalamu wa Viwango na wa Chakula wawepo hadi level ya Wilaya Kusaidia kuwatambua na kuwasaidia watengeneza bidhaa za viwango na kuwaelekeza taratibu za kukuza biashara zao nk
  • Veta zilizopo ziboreshwe zichukue wanafunzi wengi na zitoe kozi nyingi (mbali mbali katka kituo kimoja) ili Vijana wengi wapate mafunzo na hivyo kuvutia wawekezaji wa Viwanda (affordable skilled labour). Tungekuwa na Vyuo vya kutosha ningependekeza Wanafunzi wote wakimaliza Form Four wajiunge Veta kwa miezi sita ya lazima ndio utaratibu mwingine ufuate.
  • Kusaidia wafanyabiashara wa kati waweze kukua na kuongeza Ajira na Kulipa Kodi kubwa (Trickle down effect)
Ni mtazamo wangu.…
 
Kabla ya yote waniajiri kwanza Mimi mhitimu wa chuo kikuu wa 2015 katika kada ya ualimu masomo History na kiswahili.
 
Unalosema ni kweli. Ila ni muhimu kwanza kwa kuboresha mifumo ya Taasisi za kiserikali zinazochota hela kabla hujaanzisha kiwanda unakuta mtu akiwa na nia lazima atapita huku kotea Anahitaji kupita kwenye Taasisi kibao zote zinachota hela mfano
Brela, Kujisajili
Halmashauri, Leseni
TFDA ,kibali kama ni bidhaa ya chakula au dawa
TBS, Ubora wa bidhaa
TIC, Kituo cha uwekezaji
wizara husika, kutegemea na bidhaa
Ardhi, kupata kibali kujenga
mipango miji, kupata kibali
mtendaji na mwenyekiti kutambulika
watu wa Bonde, Kupewa maji
Idara ya Maji, kupata maji
Tanesco, kufunga umeme
Osha, usalama wa wafanyakazi
NEMC, kibali cha mazingira

Just imagine hizo taasisi zote upite kweli na zinatoa hela sasa hadi unaanza kazi ushafilisika hata huo mkopo ulokopa kwa riba nafuu

,
 
Kwa mtazamo wangu Mama anafanya Vizuri sana na pia najua kuwa sio kila kitu kinaweza kufanyika kwa wakati mmoja hata hivyo nimeona nichangie yafuatayo;
Ili kuboresha makusanyo ya Kodi na kutengeneza ajira nyingi kwa Vijana nafikiri ipo haja ya kutazama upatikanaji wa Mikopo mikubwa ya riba nafuu kabisa (hii mikopo ya ndani ya riba 17 - 20% siamini kama inaweza kutuvusha)
Namaanisha kuanzisa Miradi itakayo ajiri watu wengi, yenye faida na inayo ingizia Serikali Kodi kubwa kwa mfumo wa trickle down effect

Tunaweza kuanza kwa kuforcus kwa bidhaa tunazo nunua Nje kwa wingi; Mfano:
  • Viwanda vya madawa ya watu na Kilimo (tunao wakemia wazuri waliosoma vizuri naamini tunaweza) Nafikiri ndani ya miaka 3-5 hivi hela ya Uekezaji itakuwa imerudi
  • Kiwanda cha kisasa cha kuzalisha matairi ya aina zote kama ilivyokuwa General tire ILA more innovation inatakiwa hapa kwani technology inabadilika. Soko kubwa tunalo nikuamua tu...hata sijui tunakwama wapi
  • Kiwanda kuzalisha Lami/Kusafisha mafuta (tunahitaji Lami, mafuta nk) kwa bei rafiki
  • Kuchakata gasi tuliyo nayo ifae kupikia au pengine kusambaza gesi tuliyonayo kwa watu
  • Kiwanda Kikubwa na cha kisasa cha kutengeneza genuine spae kama ilivyo kuwa Machine tools ILA hapa tunahitaji kiwanda cha kisasa zaidi kiendane na wakati
  • Meli ya kisasa za Uvuvi kwani tuna ukanda mkubwa wa bahari ila hatufaidiki nao
  • Kilimo cha Mazao ya kimkakati na Ranchi za shamba darasa (namaanisha shamba la kuanzia hekari 100 hivi nakuendelea. Tunao Vijana wengi wazuri wa kila idara ya kilimo kutoka pale SUA nk.
  • Kiwanda kikubwa cha Vifungashio vya bei rafiki na wataalamu wa Viwango na wa Chakula wawepo hadi level ya Wilaya Kusaidia kuwatambua na kuwasaidia watengeneza bidhaa za viwango na kuwaelekeza taratibu za kukuza biashara zao nk
  • Veta zilizopo ziboreshwe zichukue wanafunzi wengi na zitoe kozi nyingi (mbali mbali) ili Vijana wengi wapate mafunzo na hivyo kuvutia wawekezaji wa Viwanda (affordable skilled labour)
  • Kusaidia wafanyabiashara wa kati waweze kukua na kuongeza Ajira na Kulipa Kodi kubwa (Trickle down effect)
Ni mtazamo wangu.…
Mawazo mazuri sana. Changamoto itakuja kuwa kupambana na importers wa hizo bidhaa.
 
Hiyo Mikopo ni kwa ajili ya kulipa mishahara na posho, isitoshe Tanzania kuna uchumi gani huo wa ku stimulate ?
 
Back
Top Bottom