Mikopo ya M-Pawa (M-PESA)

Mikopo ya M-Pawa (M-PESA)

MwakiIV

Member
Joined
Aug 31, 2018
Posts
79
Reaction score
138
Binafsi ni mtumiaji wa Vodacom na nimekutwa nishawishiwa kupewa mkopo wa 162,000/- wa M-Pawa.

Siku niliyojaribu nilipewa pesa nisiyojua ni sh ngap kwa maana nilioneshwa salio jipya na nilipojaribu kutafuta difference na salio langu la awali bado nikapata kama 130,000 hivi.

Swali ni je hawa wanaokopesha digitali 160,000 na mteja akapewa 130,000 kisha kutakiwa kulipa 160,000 riba 30,000/mwezi wamejisajilije?

Kwa nini mifumo mingi ni kama inanyonya sana watanzania?

Ukweli ni kwamba walio wa chini ndio wataangaika ni mikopo kama hii. Viongozi wafike sehemu watizame maslahi mapana ya wananchi.
 
Back
Top Bottom