maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,311
- 15,640
Nimeskia redioni TCRA wanasema hawahusiki na hiki kinachoendelea kwenye mikopo mitandaoni. TCRA mnaweza kuwa hamuhusiki kweli ila na nyie pia mmezembea sana kama wenzenu BOT licha ya makelele mengi kuhusu hawa mikopo mitandaoni ambao wengi hawajajisajili na wala hawana physical address.
kwanza jina lenu linatumika sana na hawa mikopo mitandaoni kuwa mnashirikiana nao na mpo kimya hamjakemea. Pili hamjaonesha hatua yoyote ya kudhibiti hili ikiwemo tabia ya hawa wakopeshaji kusajili line za simu zaidi ya 20 ili kutukana na kudhalilisha watu.
Na tayari imeonekana kuwa hizi line nyingi ambazo wanatumia kutukana watu wamezisajili kwa kutumia vitambulisho vya wateja wao, kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa mteja aliekabidhi data zake.
Tatu hamjachukua hatua zozote kudhibiti hizi Apps licha ya BOT kutoa muongozo ambao nao hawajachukua hatua zozote zaidi, ila nyie mngeshachukua hatua kwa upande wenu.
Mngeshachukua hatua za dharura ili watu wazireport hizo namba kwenu kwa hatua za kiuchungizi au kudhibiti.