| | |
| | |
| LABOUR, EMPLOYMENT AND YOUTH DEVELOPMENT | Security | 22 June 2011 |
| | |
| | |
| | |
| | |
[TD="colspan: 5"]
[TD="width: 10%"]
[/TD]
[TD="width: 90%"]
Muhama, Abia Nyabakari[CCM]
Special Seat
[/TD]
[/TD]
[TH="width: 11%, align: center"]
Session No
[/TH]
[TH="width: 16%, align: center"]
Question Number
[/TH]
[TH="width: 41%, align: center"]
To the Ministry of
[/TH]
[TH="width: 16%, align: center"]
Sector
[/TH]
[TH="width: 16%, align: center"]
Date Asked
[/TH]
[TD="align: center"]4[/TD]
[TD="align: center"]103[/TD]
[TD="colspan: 5"]Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri aliyonipatia, lakini bado nina maswali mawili ya nyongeza:-
(i) Kufuatana na hali ngumu ya maisha iliyopo sasa inayowakumbuka wastaafu hao na wengine hufa hata kabla ya wakati wao; je, Serikali ipo tayari kumpa mstaafu huyu posho ya kila mwezi kufuatana na cheo alichokuwa nacho kama aliyeko madarakani sasa kama angestaafu leo?
(ii) Shirika la NSSF limepanga mikakati gani ya kumkopesha mteja wake kwa sababu ana kianzio cha kumdhamini katika shirika hilo? Je, Serikali ipo tayari kufanya hivyo kwa ajili ya maandalizi ya kustaafu kwa mfanyakazi huyu ili aweze kumudu maisha yake binafsi baadaye?
[/TD]
[TH="colspan: 5, align: left"]
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 103 SESSION # 4
[/TH]
[TD="colspan: 5"]
[TD="width: 10%"]
[/TD]
[TD="width: 90%"]
Answer From Hon.
Mahanga, Dr. Milton Makongoro
LABOUR, EMPLOYMENT AND YOUTH DEVELOPMENT [/TD]
[/TD]
[TD="colspan: 5"]NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA:
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kazi na ajira, ninapenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Nyabakari kama ifuatavyo:-
Hili la kwanza kwamba, mfanyakazi au mwanachama ambaye yupo kazini, apewe posho huku akiendelea kupata mshahara wake, sidhani kama ina mantiki, kwa sababu yupo kazini anapata mshahara wake. Hii maana yake ni kwamba; ni akiba ya uzeeni, baada ya kustaafu au baada ya kufariki. Kwa hiyo, ninadhani malengo siyo kumpa mshahara au posho sasa hivi wakati bado anapata mshahara wake akiwa kazini ni baada ya kustaafu. Kwa hiyo, ninadhani hili lingeendelea.
Swali lake la pili, ninadhani lina mantiki kwamba, hawa wanachama wangepewa mikopo wakiwa bado kazini ili kuwaendelea. Hili ninajibu kwamba, Shirika letu la NSSF nimeliona na ndiyo maana limeshaanza kuangalia uwezekano kwa kupitia SACCOS za Wanachama kwenye maeneo yao ya kazi, kuwakopesha kupitia SACCOS na hili limeanza kufanyiwa kazi. Lingine ni kwamba, Shirika linaangalia utaratibu wa kuwakopesha wanachama wake waweze kujenga nyumba kwa kupitia katika mamlaka, baada ya mamlaka ya NSSF kuweka utaratibu kwamba, tunaweza tukawakopesha Wanachama mikopo ya kujenga nyumba, lakini hii inahitaji utaratibu ambao unatakiwa udhaminiwe au uidhinishwe na mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa hifadhi za jamii. Pindi hili likifanyika, NSSF itaangalia uwezekano wa kuwakopesha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, yaani michango yao ile iwe ni dhamana ya kuweza kukopeshwa katika mabenki mbalimbali.[/TD]