HPAUL
JF-Expert Member
- Jan 18, 2011
- 410
- 567
Klabu ya Yanga imekuwa na mfululizo wa mikutano na mchezaji wao Mayele, mchezaji ambaye tumeaminishwa bado ni hatimiliki ya Yanga kwa mwaka mmoja ujao. Hivyo basi Yanga ina mamlaka ya kumtumia Mayele kwa mshahara wanaomlipa sasa kwa mwaka mmoja ujao. Na walishafanya hivyo kwa Fei Toto kwani walikuwa wanammiliki wao.
Yanga kama bado wanahitaji huduma ya Mayele ni kuzieleza timu zote zilizoleta offer kwamba Mayele hauzwi, na mawakala wa Mayele nao waelezwe hauzwi kwa bei yoyote na Mayele atatumikia mkataba wake kwa mwaka mmoja ujao.
Endapo Mayele anataka kuongezewa mshahara sasa hivi, kwa kuaminini kuwa thamani yake imeongezeka, Yanga ndio wameshikilia mpini, wanaweza kukubali au kukataa, na maamuzi yoyote Yanga watakayo chukua hayawezi kuvunja mkataba kama kweli wana mkataba naye.
Endapo Yanga itahitaji huduma ya Mayele baada ya mkataba wake Kwisha, itabidi Yanga imwage mpunga mrefu wa kushindana na waarabu, kwani Mayele mwenyewe amesema Wa Congo wanapenda pesa.