Kwa mara ya kwnza tunashuhudia upinzani wa aina yake nchini Tanzania, upinzani ambao unaacha kupigana na utawala uliopo na badala yake unapigana na kivuli cha marehemu Magufuli.
Naomba ieleweke kuwa hili halitokei kwa bahati mbaya, Zitto Kabwe kukejeli ndege zilizonunuliwa na Serikali ya awamu ya tano, si kwa bahati mbaya, Tundu Lissu kumsema vibaya Magufuli na uongozi wake ni mkakati wa kuua kabisa legacy aliyoiacha ili aliyepo aweze kung'ara maana bila hivyo anaonekana hajafanya kitu.
Haya yanayoendelea ni utekelezaji wa kinachoitwa "maridhiano" ya 'scrach my back I scrach yours' vyama vya upinzani vimeingia maridhiano ya kusaidia utawala uliopo ili na wao waweze kulegezewa maisha yao yaende.
Naposema maisha yao yaende muelewe kwamba upinzani haujawahi kuwa kwaajili ya kusaidia wananchi bali wananchi ndio wanaowasaidia kutimiza malengo yao ya kuitisha Serikali na kuweza kuitwa Ikulu kupewa vibahasha (hii waliikosa kipindi cha awamu ya tano) .
Hii inayoitwa nguvu ya umma ndiyo mtaji wa vyama vya upinzani kujaza matumbo yao. Mbowe anapoonekana kuwa na ushawishi wa watu wengi basi lazima Serikali itamwogopa na kumwita mezani hali kadhalika Zitto na wachumia tumbo wengine.
Watanzania tusitarajie kipya katika mikutano hii ya hadhara zaidi ya kusikia Magufuli alifanya baya hili na lile, wanalipa bili kwa aliyewapa kazi hiyo na wanafanya hivyo wakijua Watanzania watasema ni kwasababu Magufuli aliwabana hivyo wanalipa kisasi lakini ukweli ni zaidi ya kulipa kisasi. Wanalipa bili.
Yapo mambo mengi sana yanayotokea sasa hivi ambayo upinzani unapaswa kusaidia kuyasemea lakini wao wamebaki kumshambulia Magufuli ambaye masikini wa Mungu kajipumzikia.
Mfano mzuri mtakumbuka huyu Zitto wakati wa nyuma alikuwa mkosoaji mkubwa sana wa kuongezeka kwa deni la Taifa, hakuna bajeti iliyokuwa inapita bila Zitto kuonya na kufanya analysis kuhusu kuongezeka kwa deni la Taifa, lakini kama walivyosema wahenga njaa ikiamia kichwani ni mbaya, sasa hivi Zitto amekuwa muimba mapambio na wala hazungumzii kabisa kasi ya ongezeko la Deni la Taifa kipindi ambacho hata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Geterres, ameonya kuwa madeni ndiyo yanayozimaliza nchi za Afrika
Zitto yupo kimya kipindi ambacho alipaswa kupiga kelele kama mwehu, kuliko ambavyo aliwahi kufanya huko nyuma, ila kwasababu tu ya kuwa kwenye payroll ya nyumba nyeupe, ameacha na anawahadaa Watanzania kwa kusema ndege zina kutu lakini hasemi vipi kuhusu zilizoagizwa na Serikali ya awamu ya sita ambazo nazo ni matoleo hayo hayo.