Mila ya ‘kumaliza msiba’ inavyowatesa wanawake Mara

chai
 
Mila za watu ziheshimiwe la muhimu wapime ukimwi na magonjwa ya zinaa kisha kazi iendeleee
 
Basi wapime ukimwi na mangonywa ya zinaa kwanza
 
Watu wengine wanaweza wasiamini lakini hiyo mila ipo, kwa zama hizi mila ya aina hii itatekelezwa na watu ambao hawajaenda shule na bado wanaamini katika mila na mizimu.
 
Magazeti bana


Kuna mambo ya msingi na ya maana sana ya kuandika lakini Kwasababu wanaogopa MaCCM wanayakwepa.

Yamebaki kuchonga na kutafuta vijiagenda vya kipumbavu pumbavu kila siku.

Mimi kwetu Mara na sijawahi kusikia hiki kitu.

Na possibly unaweza kukuta ni siyo utamaduni wa kabila ila ni utaratibu wa familia moja lakini hivi vijigazeti vinaandika as if ndio mila, utaratibu na desturi za makabila ya Mara
 
du!!!!...ngoja nihamie tarime!!!!
 
Kwetu UJITANI haimhusu mjane tu,bali na mgane pia ina mhusu. Kwa hiyo suala la kumnyanyasa mwanamke kwa hii mila potofu halipo UJITANI.

Lkn,nadhani sasa inatokomea ijapo nina miaka mingi sana bila kujiridhisha ila mwaka 2004 rafiki wa kaka yangu alifiwa mke na ili mbidi kutafuta mwanamke wa kuzugia mara moja tu miezi miwili baada ya kifo cha mkewe.

Tukiwa wawili tu usiku ndani ya boti ya kuvulia samaki ziwani jamaa ndipo akawa ananisimulia na akanieleza kuwa unalazimika kwenda kwa mwanamke asiye jua kuwa unataka kumaliza msiba kwani akijua hawezi kukubali ng'o.

Lipo na suala la kufiwa mtoto,wazazi wa mtoto lazima mmalize msiba,sasa hili sina ushahidi nalo lkn UJITANI KWETU enzi zile lilisemekana kuwepo ila likiwahusisha wazazi wa mtoto aliyefariki tu.

Sasa ikiwa mtoto kafariki wakati wazazi walishatengana ndipo hutokea sokomoko hapo.
 
Wajita hawana hizo Mila acha kupotosha, Mila iliyokuwepo Kwa wajita huko zamani ilikuwa ya mke wa marehemu kurithiwa na ndugu wa marehemu, sasahivi nayenyewe ilishaisha
Ilikuwepo mkuu ila haikuwa na nguvu na wala hatengwi mtu wala hafuatiliwi kwa ajili ya uthibitisho. Kurithi mke pia haikuwa na nguvu sana labda mme afariki wakati mjane bado ni mbichi.

Atarithiwa na siyo direct,kaka au mdogo wa marehemu anakabidhiwa kutunza familia ya marehemu kwa kila hali km ilivyo familia yake.
Sasa mmoja wao ama wote wanajiongeza na kuendelea kumbakisha mke wa marehemu ndani ya himaya na kuendelea kuzaa watoto ndani ya familia ya marehemu.

Ila baada ya magonjwa kuzidi,elimu kupanuka hakuna hayo mambo tena.
 
Niko Mara na mi ni mjita ila hii yako leo ndo naisikia,
Au na we umeadithiwa bob
Kuiskia kwa mara ya kwanza haimaanishi kuwa haipo. Anzia hapo kufuatilia utapata ABC, kwa sababu ya uelewa kwenye jamii kuanza kuongezeka, haya mambo yanafanywa kwa siri na wazee wachache wanasimamia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…