Milango na Madirisha

Jamestanzania

Member
Joined
Oct 21, 2022
Posts
21
Reaction score
11
Msaada wenu namna ya kumpata mdau ambae ana tengeneza milango halisi ya mninga.'

Asanteni.
 
Kuna wauza milango sio poa kabisa. Nilinunua mlango jamaa akanambia huu ni mninga. Nikamwambia mbona Albino,Wema sepetu na konde boy wamo humo?

Jamaa akasema hio mix ya mninga halisi, kutokana mimi si mtaalamu wa mbao nikabeba. Nimeweka kwenye nyumba baada ya miezi sita mlango umekuwa kama Chidi Benz nikasema hapa nimepigwa🤣🤣
 

[emoji23][emoji23]ndio nacho ogopa mkuu. Pole sana.
 
Wadau, mwenzenu bado ninaumiza kichwa ni wapi nitapata mafundi wazuri waaminifu wa milango ya mninga na frame zake.
Kuna watu humu ndani mmesha pita hizi hatua na mnawafahamu mafundi, tafadhali tusaidiane.




Nazungumzia milango mizuri kama hii.
 

Attachments

  • IMG_2074.jpg
    38.8 KB · Views: 7
Ungeweka na location yako ili usaidike kirahisi.
 
Asante sana. Niko Moshi Kilimanjaro mkuu.
Nchi yetu ni nchi ya ajabu sana. Kwenye kila ufundi wengi ni matapeli au hawana ujuzi. Nakumbuka siku za nyuma kuna fundi alishakimbia na mbao zetu za mninga. Au wengine wanaweza kukubadilishia. Na wengine unakuta hawana ujuzi wanaharibu na hawana fedha ya kulipa. I hope utapata members hapa watakumbia lakini uwe makini sana kwani hapa pia wapo matapeli.
 

Mkuu nakushukuru sana kwa ushauri wako. Utapeli ndio ninao ukimbia. Nimatumaini yangu nitapata msaada hapa kwenye hii forum.
 
Kama ungekuwa DSM ungewacheki hawa jamaa. Wapo vizuri na waaminfu sana
 
Tafute watu wa furniture kabisa sio mafundi wa mchongo ...Dar wapo kibao ila uwe makini tafuta wale wenye ofisi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…