Tetesi: Milestone International Co. Ltd iliyolipwa Milioni 866.6 ni kampuni ya Mbowe inayosimamiwa na shemejiye Kineneko Mtei

Tetesi: Milestone International Co. Ltd iliyolipwa Milioni 866.6 ni kampuni ya Mbowe inayosimamiwa na shemejiye Kineneko Mtei

Status
Not open for further replies.
Joined
Dec 10, 2017
Posts
57
Reaction score
143
Kwanza naomba kwa heshima na taadhima, admin msiunganishe uzi huu na mwingine.

Ndugu wanajukwaa, kama wote tupendavyo, juhudi za kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya kodi za watanzania ni endelevu na popote pesa hizo zinapokwenda sisi watozwa kodi lazima tuhoji.

Nimeona uzi huku ndani
Hivi ndivyo Freeman Mbowe na genge lake anavyotafuna pesa za CHADEMA!

unaozungumzia ripoti ya CAG kwa mwaka 2016/17ambayo pamoja na mambo mengine inazungumzia pesa zilizolipwa M/S Milestone International Co. Ltd kiasi cha 866,600,000. Kumbuka malipo haya ni kwa mwaka mmoja wa 2016, hatujui miaka mingine ya nyuma, na 2017 na 2018.

Nilichotaka kuonyesha ni kuwa kampuni hii mmiliki wake ni Freeman Mbowe, na Managing Director ni Shemeji yake wa kike aitwaye, Kineneko Mtei mdogo wake Dr. Lilian Mtei, mke wa ndoa wa Freeman Mbowe.

Kwanza hapa kuna mgongano wa maslahi na harufu ya rushwa, haya machache ni kwa mujibu wa ripoti ya msajiri pale penye mashaka, kwa kweli CHADEMA kuna ufisadi, otherwise wangeweka wazi ripoti yao ya fedha wazi tuone matumizi yao kwa ujumla na wanaofaidika na kulipwa pesa hizo.

========

CHADEMA wamekanusha hii habari.

=========

Naomba kutoa ufafanuzi ufuatao kuhusu Kampuni ya Milestone kuhusishwa na Mhe.Freeman Mbowe kama ifuatavyo;

1. Mhe. Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA sio mmiliki na wala sio mjumbe wa bodi wa Kampuni tajwa na Hana maslahi nayo binafsi ya kifedha wala kibiashara.

2. Mhe.Freeman Mbowe sio mwanahisa na hajawahi kumiliki hisa za Kampuni ya matangazo ya Milestone kama ambavyo mwandishi mtoa tuhuma ametaka kuuaminisha umma kwenye andiko lake.

3. Mhe.Freeman Mbowe sio yeye aliyeingia mkataba na Kampuni ya Milestone ila ni Chama kilifanya hivyo mapema 2015 kabla ya Kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2015 na hii ilikuwa baada ya kushindanisha makampuni kadhaa ya kutoa huduma za matangazo yaani Billiaboards na hatimaye Kampuni hii ikashinda zabuni husika ya kuweka mabango ya mgombea Urais wa UKAWA 2015 nchi nzima.

Kampuni hii ilikuwa na unafuu ukilinganisha na nyingine ambazo ziliomba zabuni husika ya kufanya kazi hiyo.

4. Tunamtaka mwazilishi wa tuhuma hizi atoe uthibitisho wowote alionao kuwa Kampuni hii inamilikiwa na Freeman Mbowe na sio kutoa tuhuma za jumla zenye lengo LA kuchafua watu na Chama kwa manufaa ya kipropaganda na yenye lengo ovu.

Mwisho, tunaishauri JF iweke utaratibu wa kuwataka uthibitisho Wanachama wake pale wanapoandika tuhuma nzito na zenye kuchafua watu binafsi na au taasisi kabla ya kuandika tuhuma nzito kama hizi.

CHADEMA tutaendelea kuwa imara Katika kusimamia matumizi bora ya rasilimali za taifa letu. Nawashukuru kwa ushirikiano.


John Mrema -Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA
 
Subiri uone watakavyomtetea Mbowe. CHADEMA kama sikio la kufa, hawajiulizi ni kwanini chama kimekuwa katika madeni yasiyoisha wakati hata ofisi hakuna. Kuwa na deni siyo dhambi ila madeni ya CHADEMA fedha zinaenda wapi? Ofisi hakuna, kila siku wanachangishana kulipia nini sijui? Na hapo hujataja zile fusso chakavu walizouziwa.
 
Subiri uone watakavyomtetea Mbowe. CHADEMA kama sikio la kufa, hawajiulizi ni kwanini chama kimekuwa katika madeni yasiyoisha wakati hata ofisi hakuna. Kuwa na deni siyo dhambi ila madeni ya CHADEMA fedha zinaenda wapi? Ofisi hakuna, kila siku wanachangishana kulipia nini sijui? Na hapo hujataja zile fusso chakavu walizouziwa.
Soma hiyo mbona mnaitetea wakati hata international community imeshaweka saini? Kwanini la Mbowe uone la ajabu?
AFRICA’S NEW DICTATOR: Tanzania’s President John Magufuli bans Opposition Politicians from Politics
 
Basi nchi hii tuna bahati mbaya. Kama kweli CDM kuna mazezeta, nadhani mazezeta zaidi wako upande mwingine, kiongozi hajui Kiswahili, hajui Kiingereza sasa mnajuaje kama anajua mambo mengine? Nyie ndo Mazezeta squared
hata kabila lake for certainty halijulikani....
 
Nadhani ungeweka ushahidi kuhusu umiliki wa hiyo kampuni, sio kusema tu inamilikiwa na Mbowe bila ushahidi.

Kama hauna ushahidi katika hilo basi muache Mbowe ale maisha tu.

Hata yule Msukuma wetu anakula maisha wakati majumba kibao ya serikali aliuza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom