Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kwa siku sita sasa, wakazi wa Buza tunaendelea kuishi katika mazingira hatarishi baada ya taka kurundikana katika maeneo mbalimbali bila kuondolewa na mamlaka husika.
Gari la kukusanya taka linalosimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke lilipita mtaani likitoa tangazo kuwa wakazi watoe taka nje kwa ajili ya kubebwa. Hata hivyo, tangu tangazo hilo litolewe, taka hizo zimeendelea kubaki mitaani huku nyingine zikisambaa barabarani na mbele ya nyumba kutokana na kuchelewa kuondolewa.
Hali hiyo imesababisha harufu kali na mazingira yasiyo salama kiafya, huku wananchi wengi tukiwa na hofu ya kuibuka kwa magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafu huo kuendelea kuwepo karibu na makazi yetu.
Wakija wanatuambia tutoe taka nje kwa sababu gari linapita, lakini mwisho wake tunakaa nazo karibu wiki nzima.
Taka zinamwagika kila kona na watoto wanachezea karibu na uchafu huu.
Wananchi tunasema hali hiyo imekuwa ya kawaida, licha ya kucheleweshwa kuondolewa kwa taka, bado Mamlaka hukusanywa fedha za usafi kiasi cha shilingi 3,000 kila mwisho wa mwezi.
Tunajiuliza hizi fedha tunazolipa ni kwa ajili gani kama mazingira yenyewe yanazidi kuwa machafu kila siku.
Tunazitaka mamlaka za Temeke Municipal Council kuchukua hatua za haraka kuhakikisha taka zinaondolewa kwa wakati ili kulinda afya za wananchi na kurejesha mazingira salama katika maeneo yao.