Haya maigizo ya Aziz Kii na Hamisa Mobeto hayana kabisa afya kwa klabu yetu ya Yanga, na hasa kipindi hiki cha kuutetea ubingwa wa Ligi kuu na ule wa kombe la shirikisho la CRDB!
Shida kubwa timu ikifanya vibaya, au hata yeye Aziz Kii mwenyewe ikatokea akacheza chini ya kiwango kwenye baadhi ya mechi, maadui zetu watapata cha kusema! Haya mambo alitakiwa ayafanye wakati wa mapumziko baada ya msimu wa Ligi kufikia tamati.