Milion 3 biashara gani naweza kufanya?


Hizo mil.3 umekopa au unazo mkononi?
 

Mama Derick; kuhusu incubator sifikiri kama kuna haja ya kuagia toka China, nenda SIDO watakuunganisha na watengenezaji wa incubator wa hapa nchini. Nimekuwa nikiziona katika maonyesho ya biashara (sabasaba) na hata kwenye nanenane. Nitajaribu kutafuta contact zao kwani nilichukua vipeperushi.
 
Kwakuwa uko serikalini na asilimia kubwa wanakipato kidogo si haba ukawatangazia kuwa unakopesha fedha kwa riba ya asilimia 10 kwa mwezi na kiwango kisizidi laki mbili kwa mtu so unazikopesha mwanzo wa mwezi kwenye msahahara wanakurudishia nadhani itakulipa zaidi kuliko we fikiria kwa kila mwezi unafaida ya Tsh 300,000/= kwa miezi kumi 3m unayo ni biashara gani utafanya kwa mtaji huo upate faida kama hii achana na mawazo mgando mara fuga kuku,kitimoto,karanga,nwea pombe nk nk
 
biashara ya pikipiki ina mambo mengi sana yanaweza kuku-discourage kuna mtu hapo juu ametoa mchanganuo wa kipato bila kupiga hesabu ya gharama za uendeshaji kama services, vifaa kuharibika n.k na pia pikipiki (za kichina) zina life span fupi sana kabla ya kuanza kusumbua. Naongea kwa uzoefu maana mke wangu ana hiyo biashara na ana pikipiki 4 na ile yenye kubeba mizigo moja ila hicho kizunguzungu cha uendeshaje wake ni balaa na pia unatakiwa kuiuza mara moja inapoleta matatizo na watu uwa wanalalia sana wakati wa kuzinunua zikiwa used. Unaweza kufanya hiyo biashara ila ni ngumu sana na unatakiwa kuwa una-save hela yote ili uendelee ila kama mapato yake ndio unayategemea kuendeshea maisha achana nayo kabisa

Pikipiki ikikaa miezi 6 inakuwa imechoka tayari kwa hiyo unaiangalia kama bado inaingiza kipato vizuri au inakugharimu zaidi ukiona gharama ni kubwa au faida ni kidogo uza nunua nyingine na mshauri alisema kuwa inaweza kaa mwaka 1 na nusu hiyo ni ngumu maana ikifika mwaka tu inakuwa imechoka sana

Sikushauri kununua pikipiki ni biashara ngumu sana na ushindani ni mkubwa saba pia ajali ni nyingi mno unaweza kukuta zimegongwa au kuanguka ikawa right off na huyo dereva akakugharimu kumtibu mie naijua hiyo biashara A to Z na mke wangu ameifanya zaidi ya miaka miwili sasa mwanzo zilikuwa zinalipa wakati ziko chache ila kwa sasa anataka kuacha maana imekuwa biashara kichaa
 
Ungekuwa unaweza ungekuja huku kanda ya ziwa, kwani kuna opportunities nyingi tuu (ila zinatafunwa na wajanja kutoka kenya, uganda rwanda, china etc) kama vile biashara ya kununua na kuuza dhahabu, almasi, silver etc yaani unanunua wewe mwenyewe kwa wachimbaji wadogo wadogo alafu unasafirisha Dar, Nairobi, Kampala au hata abroad (kama mtaji ukikua) kwa kweli biashara hii imewatoa vijana wengi sana! tena wengi wao walianza na mtaji mdogo tuu, ila inahitaji your full involvement, kujishusha na umakini wa hali ya juu
vile vile kuna uvuvi wa samaki ( sato & sangara) especial ukiwa na boti mbili tatu hivii, kwani kuna viwanda vinanunua kwa kilo (up to 2$ per Kg depend on fish qualities), biashara ya mifugo ( mbuzi, kondoo, ng'ombe etc), Asali, nta, etc
 
Wakuu tusisahau kwamba mtoa Mada ana 3M (Milioni Tatu Tu)..., tukitoa ushauri tuzingatie hilo.
 

nashkuru sana mgombezi,bs naomba untumie contact zao kama ukipata ivo vipeperushi
 

Mama ushauri wangu bora uzingize kwenye kilimo huko iringa kuna mazingira mazuri ya kilimo hebu fanya utafiti wa kilimo kilimo kinatoa watu unaweza kulima vitungu vinasoko unaweza angalia mazao yoyte kulingana na Aridhi iliyopo sehem unayoishi
 
We zinywe pombe tu, make hizo huwezi kufanya chochote. ukilazimisha kufanya biashara yoyote haziwezi kutoka make ni kidogo sana

hakuna mtaji mdogo, hata buku inatosha kuwa mtaji mkuu
 
Mama ushauri wangu bora uzingize kwenye kilimo huko iringa kuna mazingira mazuri ya kilimo hebu fanya utafiti wa kilimo kilimo kinatoa watu unaweza kulima vitungu vinasoko unaweza angalia mazao yoyte kulingana na Aridhi iliyopo sehem unayoishi

nashkuru kwa mawazo yako mkuu
 

thanx funzadume kwa mfano wako hai.bora nimejua mapema..thanx
 
please ni PM with the details za hii machine,na inapatikana wapi in China
 
biashara ya boda boda,bima yenu inachukua muda gani kucompesate pikipiki iliyoibiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…