Kama haupendi biashara ya mboga mboga na boda boda, basi nunua mshine ya juice pale university of Dar es salaam, inauzwa milioni moja na nusu. Nenda sido lipa laki mbili na nusu soma wiki 2 jinsi ya kutengeneza juice. Mashine inatengeneza lita mia moja kwa saa. Uwiano kama ukitengeneza maembe ya shilingi elfu mbili na mia tano, utauza na utapata shilingi elfu kumi na tano kwa kuuza kila glass au robo lita shs mia tano. Kama una mtoto wa kiume au wa kike ambaye si mlevi, mtume akanunue alizeti magunia mia moja. Kila gunia moja litakupatia faida ya shilingi elfu ishirini. 20,000 x 100 = 2,000,000/= Magunia mia utayapata kwa shilingi milioni mbili. Nimekwisha kufanyia hesabu nyingine kama vile usafiri, kukamua mafuta kwa mashine ya mtu. Kusafirisha mafuta sokoni na mwisho wa siku kwa siku 60 utakuwa na faida shilingi milioni 2, akiba yako ingelikuwa laki 4 na mtaji wako utakuwa umebaki pale pale milioni 3. Utakuwa umekwishajilipa mshahara pia hata kama umeajiriwa. Kwa mawazo zaidi, 0718 19 4606. Mwalimu wa ujasiriamali. Nitakuchaji shilingi elfu kumi ushauri kwani wewe ni mwana JF. Usisahau kukata bima kama utaamua kufanya biashara ya boda boda. Ukinitumia mimi nitakuuzia pikipiki na utakata bima shs 72,000 majambazi wakikunyanganya au ikipata ajali tunakupa pikipiki nyingine. Jamaa alioandika biashara ya mboga mboga na pikipiki nao pia ushauri ni mzuri sana. Uchukue wowote