Pre GE2025 Milion 600 kujenga kituo kipya cha afya Mahuninga, Iringa

Pre GE2025 Milion 600 kujenga kituo kipya cha afya Mahuninga, Iringa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Kutokana na changamoto ya muda mrefu wanayopitia wananchi wa kata ya Mahuninga halmashauri ya wilaya ya Iringa Mkoani ya kufuata huduma za afya umbali mrefu uenda ikabaki historia mara baada ya kutengwa kiasi cha sh milion 600 kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha afya.

Kituo hicho kinajengwa ili kusaidia upatikanaji wa huduma za afya kwa jamii ya kata hiyo na maeneo jirani ambapo takribani wananchi 6842 watapata huduma katika kituo hicho awali iliwalazimu kutembea umbali mrefu.

Pia soma: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Wakiwa katika ziara ya ukaguzi maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Isimani Amos Ndasso akiambatana na Afisa Tarafa, Tarafa ya Idodi Mapessa Makalla pamoja na Katibu wa hamasa na uhamasishaji Wilaya ya Iringa Omary Chulla wameridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo na kuagiza kasi zaidi ili mradi ukamilike kwa wakati.
1741613913945.png
 
Back
Top Bottom