Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Milionea Gathuo Gichuru raia wa Kenya amejikuta akiangukia kwenye uuzaji mitumba baada ya kufilisika kutokana na kumaliza pesa kwenye kampeni za kuwania kiti cha Senate eneo la Laikipia mara mbili bila mafanikio.
Gathuo ambaye ni mhitimu wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Kenyatta aliamua kujiingiza katika siasa baada ya kufanikiwa kwenye biashara mwaka 2013 lakini aliishia kuanguka mara mbili, 2013 na 2017 na kupelekea kuingia katika lindi na umasikini.
"Nina msongo wa mawazo, mke wangu alinikimbia 2013 baada ya kushindwa uchaguzi, ndugu zangu pia walinisaliti. Nimeamua kuwa muuza nguo ili niingize kipato", amesema Gathuo huku akiangua kilio.