Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MILIONI 16 ZACHANGIA UJENZI WA ZAHANATI 13 JIMBO LA BAHI, DODOMA
Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo tarehe 03 Mei, 2023 alifika Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe kwa lengo la kutembelea ujenzi unaoendelea wa Zahanati ya Mapinduzi ambayo ni miongoni mwa zahanati ya 13. Zahanati zote 12 zimesha na Mbunge alitoa Tsh. Milioni 16 za mfuko wa Jimbo.
Tarehe 6 Mei, 2023 siku ya Jumamosi Mbunge ataungana na wananchi wa Mapinduzi kumwaga zege kwa ajili ya kuweka jamvi. Mhe. Nollo anapenda kutoa shukurani za dhati kwa Wananchi wote wa Bahi kwa ushirikiano wanaompatia kwa kujitolea kwenye kazi za maendeleo.