Deo Corleone
JF-Expert Member
- Jun 29, 2011
- 17,006
- 13,281
Mimi nimeanza hivi.
Laki 4 na themanini nimekodi fremu kwa miezi 6,laki 5 nikanunua till ya tigo pesa Na 1 na nusu till ya M pesa,nikatenga laki 6 Kama mtaji,biashara imeanza maana Fremu haikuhitaji matengenezo.sasa hivi najipanga nipate refrigerator ili niweke vinywaji baridi then niweke vyakula Kama mchele,maharage Na unga Wa ugali.Nitajipanga liwe duka kabisa maana maeneo nlopata Fremu hakuna duka.mpaka sasa nimetumia Kama 1.8 hivi
Record keeping ucsahau, Ila hongereni Kwa graduate kuwa Na mawazo ya kujiajiri
nimewasoma wadau,laiti kama ningewapata vijana kama nyie tungeanzisha kampuni kubwa itufaidishe,tatizo la graduate wengi ni wabinafsi sana!
Ndo nimemaliza chuo this year. Ajira hazipo na kama zpo hazitatimiza ndoto zangu za kwenda brazil kucheki world cup! Chumba kitupu kipo hapa home ndo nataka iwe ofice yangu! Nitaomba kwa family 2 milions yani aprox ya mshahara wa miezi 4 ya graduate!
Yes mwanzo sio mbaya.nilichagua a good location kuna kituo cha daladala Na mama ntilie wengi.so kwa biashara Yangu naamini itafanya vizuri.
Ni kutumia fursa tu maana kuna wengne hata huo mtaji Wa 2m kuupata ni shida.
Na wengine wapo mbali kweli kiasi kwamba kwa wale waliopiga shule na wepesi kukata tamaa wanaweza kujuta kwanini walienda shule but all in all kila mtu ana nafasi ya kufanikiwa hasa ukizingatia Watz tuliowengi tuna umasikini wa kifedha tu ila kiuchumi tupo vizuri kama tutaamua kuchukua hatua tutatoka katika kiwango cha kumudu gharama za maishaSasa elimu hz tulitakiwa tuwe tumepewa tangu darasa la 7! Mwanafunzi wa darasa la 7 ambae hakupata bahati ya kuendelea angeanza hivo, sasa hv angekuwa mbali!