Huku JF kila mtu ni tajiri, amejenga nyumba ya tzs 100m kwenda mbele, sasa kuwa makini.
- Kuna watu wanauza nyumba ya vyumba vitatu kwa hiyo hiyo 35m huko Chamazi, ikiwa imekamilika, bila fensi.
Kama unalo eneo tayari;
- Kusimamisha boma hakuwezi kuzidi 10m
- Kufunika na blunder kama sio contemporary, pambania 8m, la, inakuwa chini ya hapo
- 12m iweje kwenye kuziba matundu na plumbing
- 5m itupie kwenye plaster na umeme.
Ukibana vizuri, unaweza kupiga hata white cement flani hivi.
Kama unayo 35m cash, unahamia vizuri tu, SI NDIO MAISHA yetu sisi wa hali hiyo.
Usisahau 35m hiyo hiyo, mwenzako anatungua Forester!