Milioni 4 inatosha kufungua biashara ya grocery au duka la pombe kali?

Ni wachache katika wengi. Na Hao wangefata hiyo milolongo wasingefika hapo walipo.
Sasa ukiwa hujasoma hukati leseni wala kulipa kodi? Jamaa kaandika vitu vya msingi sana. Biashara nyingi za watu ambao wana elimu duni huendeshwa kihuni kiasi kwamba asipokuwepo biashara inakufa. Hawana mifumo. Fikra kama zako hazifai.
 
Sawa mkuu nimewaelewa mil 4 haitoshi kufungua grocery mtoa Mada inabidi aongeze mtaji.
 
Huo mtaji unaweza kufanya biashara zozote kati ya hizo mbili cha msingi amua unatarget wateja wa level zipi za kiuchumi.. Ukikosea hapo huo mtaji wako hautotosha hata kununua henneesy mbili
 
Attachments

  • images (23).jpg
    images (23).jpg
    26.2 KB · Views: 27
Inatosha kabisa mchanganuo wa Grocery ni huu hapa...
1.Leseni ya biashara 80k/100k inategemea na halmashauri...
2. Liquor licence 40k
3. Kiti cha plastik 25k/50k na meza 35/50
4.Crate tupu la bia 12k/20k inategemea na location
5. Crate tupu soda 10k/15k
6.Bia kubwa TBL safari, kilimanjaro, etc bei ya jumla ni 35k/36k
7.Bia ndogo TBL safari, kili, etc bei ya jumla 30k
8. Castle lite, plisner bei ya jumla 28k/29k
9.Eagle ndogo 17k
8.Serengeti kubwa 35k/36
9.Serengeti lite 36k
10.serengeti ndogo 28k
11. Spirit ni kama ifuatavyo Highlife box 54k
12.kvant ndogo nusu 47k
13.konyagi ndogo nusu 39k
14.konyagi kati nusu 81k
15.konyagi kubwa nusu 102k
16.Redds 6@ 12k
17........
Inatosha kabisa
 
Wanaosema inatosha sijui wanatumia hesabu gani.sasa hivi kreti za soda Pepsi na coca cola kwenye gari ni elfu kumi na Tano hapo hazina maji yake.

Kreti za bia kununua kwa agent wa tbl ni elfu kumi na tatu.kwa agent wa sbl ni elfu kumi na mbili mia Tano hapo hazina maji yake.Sijajua Kwa maeneo utakayokuwepo

Shelf hujatengeneza Bado hujanunua pallet.hujaenda TRA,manispaa,cheti cha TBS,mashine ya EFD na vyeti vya afya Kwa wafanyakazi vinahitajika viwepo, vinapatikana Kwa bwana afya Kwa njia mchongo bila ya hivyo kila mara watakuja kukukagua.

Bado hujalipa Kodi ya fremu.hujanunua thamani za ofisi kama meza na viti.

Matumizi yote hapo juu Bado hujakuwa na bidhaa ya kuuza ili uingize pesa.hapo umepaki pesa ambayo haizalishi.
Zinatosha kuanzisha biashara ya vinywaji. Labda kama unataka alingame na breweries. But Kwa biashara ya jumla inatosha maana biashara ya jumla ya soda na bia haihitaji shelf, ukumbi wala viti.

TRA TIN ni bure na Ledeni ya vileo ni elfu 40 tu Kwa miezi sita. Biashara ya jumla ya vinywaji haihitaji vyeti vya Afya maana unahitaji vijana wawili tu. Moja kutoa creti ndani na kuchanganya mwingine kisukuma mkokoteni Kwa wateja wa jirani.

Kama Bado unakwama njoo ujifunze Kwa vitendo Kwa sisi tulioanza na creti Moja ya safari ndogo.
 
Labda Kwa grocery inawezekana.kwa liquor store hiyo bajeti ni ndogo mkuu.Ingawaje inategemea eneo la biashara na namna utakavyoseti biashara Yako.

Kama hutakuwa na kreti inatosha .
Hyo 4m inatosha kuanzia..
kwa jinsi ninavyoijua hii biashara hapo itategemeana na location, kama ni uswahilini hakuna shida ila kama ni maeneo ya ushuani inabidi ajiongeze afungue liquor store naona ndo zinakuja kwa kasi....

All in all I wish u all the best..
 
Wanaosema inatosha sijui wanatumia hesabu gani.sasa hivi kreti za soda Pepsi na coca cola kwenye gari ni elfu kumi na Tano hapo hazina maji yake.

Kreti za bia kununua kwa agent wa tbl ni elfu kumi na tatu.kwa agent wa sbl ni elfu kumi na mbili mia Tano hapo hazina maji yake.Sijajua Kwa maeneo utakayokuwepo

Shelf hujatengeneza Bado hujanunua pallet.hujaenda TRA,manispaa,cheti cha TBS,mashine ya EFD na vyeti vya afya Kwa wafanyakazi vinahitajika viwepo, vinapatikana Kwa bwana afya Kwa njia mchongo bila ya hivyo kila mara watakuja kukukagua.

Bado hujalipa Kodi ya fremu.hujanunua thamani za ofisi kama meza na viti.

Matumizi yote hapo juu Bado hujakuwa na bidhaa ya kuuza ili uingize pesa.hapo umepaki pesa ambayo haizalishi.
Unayosema upo sahihi, lakin hapa tunamshauri ikiwa anaanza akiwa na mtaji pungufu hivyo itambidi kutafuta vitu kwa bei ya chini zaidi(used) ..

Mfano mim kuna kipind nilikuwa na 6m nilitaka kufungua pub maeneo flan hivi, kwa bahati nzuri akatokea jamaa biashara ilimshinda hivyo alinijumlishia kuanzia kreti tupu kwa elf 8(soda na bia), stuli elfu 10 na meza ndefu, sofa za V. I. P,kaunta na shelves, TV mbil na mziki wake kwa bei ambayo ipo chini kwa kuwa alikuwa anahama hivyo sikutumia gharama kubwa sana.

NB:Kila mtu ana njia zake za kuanza biashara na kamwe huwezi kuanza na kila kitu au ukakamilisha mambo yote yanayohitajika hivyo cha msingi aanze kidogo atajiongeza mbele ya safari!
 
Zinatosha kuanzisha biashara ya vinywaji. Labda kama unataka alingame na breweries. But Kwa biashara ya jumla inatosha maana biashara ya jumla ya soda na bia haihitaji shelf, ukumbi wala viti.

TRA TIN ni bure na Ledeni ya vileo ni elfu 40 tu Kwa miezi sita. Biashara ya jumla ya vinywaji haihitaji vyeti vya Afya maana unahitaji vijana wawili tu. Moja kutoa creti ndani na kuchanganya mwingine kisukuma mkokoteni Kwa wateja wa jirani.

Kama Bado unakwama njoo ujifunze Kwa vitendo Kwa sisi tulioanza na creti Moja ya safari ndogo.
Leseni ya dukan la vinywaji elfu 40?au unaongelea leseni ya grocery mkuu.leseni haipatikani TRA ukumbuke hii inapatikana halmashauri au manispaa.baada ya kuja kukufanyia ukaguzi ikiwemo mkataba wa fremu.ukishapta hiyo ndio unakwend TRA wakupe TAX CLEARANCE huku napo wana taratibu zao za ukaguzi au urefushe mkono.makadirio Kwa biashara mpya ya vinywaji vya jumla ilikuwa ya chini milioni Tano inaanzia laki Moja na ishirini mpaka Laki nne na kitu

Yote kwa yote inawezena kikubwa ni eneo na aina gani ya biashara.yaani biashara Yako unataka ufanyanye katika hadhi gani.ila biashara yenye ubora na kwenda mitindo ya kisasa kama unavyotaka haitoshi.pia shauri za watu jaribu kuangalia huyu anakuambia alianza na kreti Moja ya safari sasa jiulize alikuwa anauza jumla au rejareja.

Inawezekana anafanya masikhara ili kuchangamsha genge, kaandika Kwa ufahamu wake akiwa timamu au kaamua kujutoa ufahamu
 
Inatosha kabisa mchanganuo ni huu hapa...
1.Leseni ya biashara 80k/100k inategemea na halmashauri...
2. Liquor licence 40k
3. Kiti cha plastik 25k/50k na meza 35/50
4.Crate tupu la bia 12k/20k inategemea na location
5. Crate tupu soda 10k/15k
6.Bia kubwa TBL safari, kilimanjaro, etc bei ya jumla ni 35k/36k
7.Bia ndogo TBL safari, kili, etc bei ya jumla 30k
8. Castle lite, plisner bei ya jumla 28k/29k
9.Eagle ndogo 17k
8.Serengeti kubwa 35k/36
9.Serengeti lite 36k
10.serengeti ndogo 28k
11. Spirit ni kama ifuatavyo Highlife box 54k
12.kvant ndogo nusu 47k
13.konyagi ndogo nusu 39k
14.konyagi kati nusu 81k
15.konyagi kubwa nusu 102k
16.Redds 6@ 12k
17........
Inatosha kabisa
Itakuwa biashara ya jumla anayouza Kwa pisi Moja moja.akija mteja wa coton hawezi kumuuzia Kwa sababu kaanza na nusu coton.

Unafahamu Kuna pub zinaagiza coton Kwa kila brand.bia Kwa mfano castle lite na Serengeti lite wanachukua Tano tano.

Weka mchanganuo kutokana na hiyo Hela.
Mtaji huo utawezekana Kwa kukwepa serikali ila akiingia kwenye mfumo w serikali atakuja hapa kuomba ushauri
 
Leseni ya dukan la vinywaji elfu 40?au unaongelea leseni ya grocery mkuu.leseni haipatikani TRA ukumbuke hii inapatikana halmashauri au manispaa.baada ya kuja kukufanyia ukaguzi ikiwemo mkataba wa fremu.ukishapta hiyo ndio unakwend TRA wakupe TAX CLEARANCE huku napo wana taratibu zao za ukaguzi au urefushe mkono.makadirio Kwa biashara mpya ya vinywaji vya jumla ilikuwa ya chini milioni Tano inaanzia laki Moja na ishirini mpaka Laki nne na kitu

Yote kwa yote inawezena kikubwa ni eneo na aina gani ya biashara.yaani biashara Yako unataka ufanyanye katika hadhi gani.ila biashara yenye ubora na kwenda mitindo ya kisasa kama unavyotaka haitoshi.pia shauri za watu jaribu kuangalia huyu anakuambia alianza na kreti Moja ya safari sasa jiulize alikuwa anauza jumla au rejareja.

Inawezekana anafanya masikhara ili kuchangamsha genge, kaandika Kwa ufahamu wake akiwa timamu au kaamua kujutoa ufahamu
Mimi nafanya. Mwaka wa Tatu huu. Mahitaji mengine ya kibiashara unatakiwa kuyashugulikia ukiwa tayari unaendelea na biashara. Mfanoi Tax Clearance unapataje wakati hufanyi biashara. Hayo mauzo Kwa siku, mwezi na Mwaka unayajuaje kama hujaanza. Hiyo Hela nyingi sana kuanza biashara ya vinywaji. Kama muoga kama wewe haitoshi but hiyo Hela inatosha Kwa kuanzia.
 
Back
Top Bottom