Milioni 5 kwa kila goli ni hela ndogo sana

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,627
Reaction score
1,926
Kwema wakuu,

Nimekaa nikawaza, TZS 5mil kwa kila goli naona kama ni hela ndogo sana. Kwa Serikali kama ya Mama Samia zile ni hela ndogo sana. Pengine hata zingefaa kua ni hela kwa kila mchezaji. Zile ni kama mshahara wa mchezaji mmoja tu hivyo hazileti sana motisha kusema unaipa timu nzima.

Serikali itoe hela za maana. Ikiwezekana ukiacha zawadi ya kila goli basi kuwe na zawadi ya kila ushindi labda 50mil au 100Mil.

Serikali haiwezi kupata hasara kutoa hata 100mil kwa timu moja ikiwa serikali inaweza kupoteza hela kibao tu kwenye issues zingine. Isitoshe timu hizi huziingizia Serikali mapato ya kutosha tu kupitia viingilio vya milangoni.

Timu zitakapofanya vizuri zikafika mbali basi hata mapato yataongezeka kupitia timu za kigeni zitakazokuja hapa kucheza na timu zetu. Toeni hela ya maana watu wafie uwanjani ingawa sio lazima sana.
 
ok toa nyingi wewe
 
Mimi naona haitakiwi kabisa kuwepo, hizo pesa wapelekewe wenye mahitaji zaidi ya hao Simba na Yanga, kama vituo vya kulelea yatima, sio kusubiri mpaka sikukuu ndio wapelekewe mbuzi, mafuta, na mchele.
 
Game sita kila game goli 2 jumla milioni 60, huu ni mshara wa wachezaji kadhaa kwa mwezi.
 
Wasitoe kabisa kuna watu wanakosa huduma muhimu katika jamii zipelekwe huko
 
Economical advantage ya timu hizi kufuzu ni kubwa kuliko hizo mil 5 zao. Kuliko zikajaze mafuta kwe ma VX au walipane posho za vikao ni heri zije zihamasishe huku.
 
Back
Top Bottom