A
Anonymous
Guest
JE, NANI ATAOKOA KAWOSA LTD KARAGWE KABLA HAIJACHELEWA?
Mimi ni mmoja wa wanachama wa KAWOSA LTD iliyopo Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera. Kwa masikitiko makubwa, sisi wanachama tunaendelea kushuhudia hali ya chama chetu ikidorora kutokana na upotevu mkubwa wa fedha za wanachama unaokadiriwa kuzidi shilingi milioni 500.
Taarifa za suala hili ziliwasilishwa kwa TAKUKURU tangu mwaka 2024 kwa ajili ya uchunguzi. Hata hivyo, hadi sasa wanachama wengi bado hawaoni hatua za wazi za kisheria dhidi ya watendaji wanaotajwa kuhusishwa na upotevu huo wa fedha. Hali hii imeendelea kutupunguzia imani katika uongozi na mustakabali wa chama chetu.
Miaka iliyopita, KAWOSA LTD ilikuwa na uwezo wa kutoa mikopo inayofikia zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa mwaka. Kwa sasa uwezo huo umeshuka kwa kiwango kikubwa, ambapo chama kinapata ugumu hata wa kufikia utoaji wa mikopo wa shilingi bilioni 1 kwa mwaka. Wakati huo huo, wanachama wengi wanaendelea kutoa akiba zao kutokana na hofu na kupungua kwa imani, jambo ambalo linaathiri ukwasi wa chama kila siku.
Tunatoa wito kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Ushirika kufanya tathmini ya kina kuhusu hali ya KAWOSA LTD na kuchukua hatua stahiki kwa wakati. Tunahitaji kuona ukweli ukiwekwa wazi, waliohusika kuwajibishwa kulingana na sheria, na hatua madhubuti zikichukuliwa kulinda akiba za wanachama.
KAWOSA LTD ni mali ya wanachama. Tunahitaji uwazi, uwajibikaji na hatua za haraka ili kuzuia chama hiki kisifikie hali mbaya zaidi ambayo inaweza kusababisha hasara kubwa kwa wanachama na jamii inayokitegemea.