Milioni 8 yako itakupa milioni 20 kwa mwaka mmoja

Biashara Kwa kuiandika inapendeza,ingia Sasa ndio utajuwa mbichi na mbovu.
 
Kuna wakati vijana hua hamjielewi kabisa, then mnakuja na nadharia za utajiri na mafanikio ya kwenye simulizi.
Sasa nikionaga upuuzi kama huu hua naishia kukasirika, mwisho natafuna meno kwa hasira tu...☹️
 
Naomba unipe chimbo la kuja kuuzia huko Dar es Salaam.
Nashangaa watu wanahangaika dubai na UK zanzibar pekee inaweza kukufanya ukawa tajiri chukua vitu vya electronic zanzibar njoo navyo dar unapiga hela.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Ni Hii Biashara ya simu ninayoijua na kuifanya mimi au unazungumzia simu aina kwa maana nyingine
 
Ushuru wa forodha hujauweka hapo.
 
Sorry ww unafanya bznes hii?



KAZI ni kipimo cha UTU
 
Post yako ipo kinadharia sana umeweka assumptions nyingi sana kuliko reality kwa mfano.
What if mteja amenunua simu kisha ikamsumbua akairudisha?
Umepigia hesabu kuwa simu zote utanunua kwa bei ya laki 1 maana yake utanunua simu za kufanana let say oppo A57 20pcs,Oppo A83 20pcs,Infinix hot 5 20pcs na wateja wakija wanaulizia Iphone 12 promax,Samsung note 20 that means hiyo stock yako uliyonunua itakaa mwaka mzima ili uzimalize na wakati huo mfanyakazi anataka mshahara wake,kodi ya fremu inaisha.
Mambo sio rahisi hivyo ingia field ndio utajua hujui
 
Katika huko kufikiria, wewe unafanya biashara gani?

#YNWA
 
Mkuu, kwa mfano UK, soko la kupata hizo bidhaa ni wapi?
 
bia$hara sio rahisi hivyo ndugu, hayo ni makadirio tu ya kwenye makaratasi.
kila mtu afanye kile anachopenda, sio kuiga kitu ambacho huna uelewa nacho wala uzoefu wa kina, utaunguza MTAJI wako bure!
NB.
biashara za NADHARIA zinalipa sana.
 
Nimefanya biashara kwa miaka 20sasa ndio natambua kuwa mafanikio NI ngumu sana kwenye biashara...Tena ukizoea biashara zenye FAIDA kubwa kubwa unafilisika chap tu...Kama una huo mtaji fungua duka la nafaka uswazi au genge mix mpaka pombe za kupima....jitoe hasa...na lugha ya ushawishi uwe nayo...
 
Biashara yoyote kwenye maandishi inalipa Sana, ingia sasa mzigoni kama ujaanza kuongea peke yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…